Wenyeviti
wa vijiji na watendaji wa ngazi zote
katika kata ya Kabilizi wilayani Muleba wameagizwa kuunda kamati ya
kudhibiti madawa ya kulevya katika kata hiyo .
Agizo hilo
limetolewa na diwani wa kata ya Kabilizi Solomoni Karuga wakati akikagua
shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazofanywa na wakazi wa kata hiyo.
Karugaba amesema kuwa viongozi hao wanatakiwa
kuunda kamati ambayo itazungukia maeneo yote ya kata hiyo kutoa elimu juu ya
madhara ya utumiaji wa madawa ya kulevya . na kuhakikisha hakuna matumizi ya
aina yoyote ya madawa ya kulevya wala kijiji kinachojishughulisha na ulimaji wa
bangi katika maeneo yao.
Karugaba
amesema kuwa kamati hiyo itakayoundwa inatakiwa kuwa inatoa taarifa kwa kila
eneo itakalokuwa inazungukia jambo
ambalo litasaidia kukomesha matumizi ya madawa ya kulevya kwani vita hiyo ni
yakila mmoja .
Hata hivyo
ameongeza kuwa baada ya kubaini kuwa
vitendo hiyo kuwa vipo kwenye kata hiyo wanatakiwa kutoa taarifa kwa diwani huyo
mara moja ili hatua za kisheria zifuatwe.
Aidha
amesema kuwa kata hiyo yenye vijiji vitano bado haijabaini kuwepo kwa matumizi
ya madawa ya kulevya au kuwepo kwa eneo linalolima bangi mpaka sasa.
Post a Comment