Wakazi wa vitongoji sita kati ya tisa vilivyoko
katika kijiji cha Bubale kata Kakunyu wilayani Missenyi, wameomba serikali
kusaidia kutatua mgogoro wa ardhi unaowakabili, ambao umesababisha kuishi
maisha magumu kwa kukosa chakula na makazi.
Wakizungumzia hali hiyo katika mkutano wa hadhara
ulioitishwa na mbunge wa jimbo la Nkenge dokta Diodorus Kamara, wananchi hao
wamesema kuwa, ugumu huo wa maisha umeotokana na makazi yao kuteketezwa kwa
moto na kufukuzwa katika mashamba yao, wakidaiwa kuishi ndani ya vitalu vya
wawekezaji.
Wananchi hao akiwemo Msafiri Sevelin na Rebeca Mussa
wamesema kuwa, mazao yao yaliyoko katika mashamba waliyolima kwa nguvu zao, kwa
sasa yanatumika kulishia mifugo, huku wakidai kuwa baadhi yao wanalala nje
kutoka na nyumba zao kuchomwa moto.
Akizungumza na wananchi hao mbunge wa jimbo la
Nkenge dokta Kamala amesema kuwa, ipo tume ambayo iliundwa na
waziri mkuu ili kufuatilia mgogoro huo wa wakulima pamoja na wawekezaji katika
lanchi ya Missenyi, na kueleza kuwa hatakubaliana na tume hiyo iwapo ripoti yao
haitazingatia mahitaji ya wananchi.
Mgogoro huo kati ya wananchi na wawekezaji katika
vitalu hivyo umeanza karibia miaka kumi na moja iliyopita, hadi sasa bado
ufumbuzi haujapatikana.
Post a Comment