Jumla ya wanafunzi 76 wa Darasa la saba katika Shule ya
Msingi Ndama iliyopo Kata ya Ndama Wilayani Karagwe wanategemea kufanya mtihani
wao wa Taifa wa kuhitimu darasa la saba tarehe 6 na 7za mwezi wa tisa mwaka huu.
Akitoa takwimu hizo mwalimu wa shule hiyo ByeraGrace Ndyanabo amesema kuwa
wanafunzi wanaotegemewa kufanya mtihani katika shule hiyo ni 76 ambapo
wasichana n i42 na wavulana ni 34
Ndyanabo amesema
kuwa wazazi na walezi wa wanafunzi hao wategemee ufaulu mzuri kutoka
kwa watoto hao kufuatia matokeo mazuri waliyoyapata katika mtihani wa
mocko uliofanyika miezi iliyopita ambapo shule hiyo ilishika nafasi ya tisa
kiwilaya kati ya shule miamoja kumi na
mbili.
Aidha ameongeza kuwa
shule hiyo inategemea kuonesha ufaulu wa hali ya juu katika mtihani wa
Taifa utakaofanyika mwezi ujao ambapo wamekuwa wakitoa majaribio ya mara kwa
mara na masoma ya ziada hali iliyofanya shule hiyo kuonesha ufaulu mzuri katika
mitihani wa mocko uliopipita na kuwapa
matumaini makubwa kwa mtihani utakaofanyika .
Hata hivyo JOHANES CHARLES ni miongoni mwa wanafunzi wa Darasa la saba katika Shule hiyo ambaye
ameeleza kuwa wanategemea kufanya mtihani huo vizuri kufuatia maandalizi
waliyoyapata kutoka kwa walimu wao ambapo pia wanatumia mda mwingi
kujisomea na kufanya majaribio ya mara
kwa mara kutoka kwa walimu wao
Post a Comment