Kamanda wa jeshi la polisi mkoani
Kagera AUGUSTIN OLLOMI amewahasa watumishi na wananchi kwa ujumla mkoani
Kagera kuacha kujichukulia maamuzi yao binafsi badala yake wawashilikishe
viongozi na familia ili kutatua changamoto zinazowakabili.
Wito huo umekuja baada ya kifo cha
kutatanisha kilichotokea Agosti 28 mwaka huu kwa askari mmoja ambaye
anakaa kambi ya Rwamishenye anayejulikana kwa jina la F1411 COPLO
MUSA SALUM MUSANYA ambaye mwili wake umekutwa unaelea maeneo ya beach ya
kiloyera iliyopo Manispaa ya Bukoba.
Kwa mujibu wa kamanda OLLOM amesema
kuwa marehemu alitoweka nyumbani kwake tarehe 25 na kuacha ujumbe mezani
unaomuelekeza mke wake jinsi ya kufungua Brificase ambapo mke wake alifanikiwa
kufungua brificase na kukuta kadi ya Benk na simu za mkononi mbili za
marehemu
Amebainisha kuwa mke wa marehemu
alifika katika kituo cha polisi mnamo tarehe 26 mwezi wa nane kutoa taarifa za
kupotea mme wake baada ya kupata mashaka juu ya mmewake kuacha mawasiliano ya
simu za mkononi na password zinazo
muelekeza kufungua brifcase ambapo jeshi la polisi lilianza kumutafuta bila
mafanikio .
.
Kabla ya mauti hayo marehemu alikuwa
amefanya kazi ya kulitumikia jeshi la polisi kwa miaka 17 ambapo marehem
amezaliwa mwaka 1973 ,mwili wa marehem unasafirishwa leo kwa ajili ya kuzikwa
Mkoani Kigoma ambapo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi juu ya kifo chake
Post a Comment