Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: HALI YA DIWANI ALIYEJERUHIWA NA WANANCHI INAENDELEA VIZURI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Hali   ya   diwani   wa   Kata   ya   Nyakahanga   Charles   Bechumila    ambaye   alijeruhiwa   katika   oporesheni   ya   kuwaondoa   ...

Hali  ya  diwani  wa  Kata  ya  Nyakahanga  Charles  Bechumila   ambaye  alijeruhiwa  katika  oporesheni  ya  kuwaondoa  watu  wanaodaiwa  kuvamia  maeneo  ya  wafugaji   katika  kijiji  cha  Kashanda  kata  ya Nyakahanga  inaendelea  vizuri  baada  ya  kupata  huduma  katika  hospitali  ya Nyakahanga.

Akizungumza  na  waandishi  wa  habari  katibu  wa  hospitali  hiyo Mchungaji   Jeremiah   Rugimbana  amesema  kuwa baada  ya  kupokelewa  alipatiwa  huduma  ikiwemo  kushonwa  pale  alipokuwa  amejeruhiwa.


Akielezea  majeraha  aliyokuwa  nayo  diwani  huyo  amesema  imeonesha  kuwa  alichomwa  na  vitu  vyenye  ncha  kali  na  kupelekea  maumivu  hayo  lakini  wanashukuru  hali  yake  inaendelea  kuimalika  na  anaendelea  vizuri.


Ikumbukwe   kuwa  msafara  wa  Mkuu  wa  wilaya  ya  Karagwe  Godfrey   Mheluka   ulishambuliwa  na  watu  wasiofahamika  kwenye  kijiji  hicho  cha  Kashanda  ambacho  kina  mgogoro  wa muda  mrefu  ambao  umeshindwa  kupatiwa  ufumbuzi  na  wakuu  wa  wilaya  ambao  wamepita  katika  wilaya  hii.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top