Wakulima
Mkoani Kagera wameshauriwa kuchangamkia fursa ya mikopo ya vitendea kazi vya
kilimo kwa ajili ya kuboresha kilimo chao na kuachana na kilimo cha kutegemea
mvua na mikono pekee.
Ushauri
huo umetolewa na Augustino Paul Ofisa Masoko wa Taasisi ya EFTA inayoshughulika
na kutoa mikopo ya vifaa vya kilimo kwa wakulima na wajasiriamali.
Paul
ameeleza kuwa Taasisi hiyo ya EFTA kwa Mkoa wa Kagera Makao yake yako katika
Manispaa ya Bukoba ambapo ameeleza kuwa Mkulima yeyote akitaka mkopo wa vifaa
vya kilimo kutoka katika taasisi hiyo wanampa elimu ya kupata mkopo na ndani ya
mwezi mmoja anakuwa ameupata.
Amesema
vifaa vya kilimo vinavyotolewa na taasisi hiyo ni pamoja na Trekta, mashine ya
kupandia(Planter, mashine ya kuvunia (Harvester , na mashine za umwagiliaji kwa
ajili ya kuongeza uzalishaji wa Mkulima na kufikia malengo ya Serikali.
Amesema
taasisi hiyo katika vifaa inavyovikopesha ni kuanzia vifaa vya million ishirini
ambapo katika marejesho mkopaji anapewa muda wa miaka mitatu kuwa amemaliza mkopo
huo wa vifaa na ambapo amesema kuwa anaamini katika muda huo mkopaji anakuwa amemaliza
marejesho yote.
Post a Comment