Na:
Sylveste Raphael
Waziara wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako katika ziara yake ya siku mbili Mkoani Kagera
kuanzia Februari 13 hadi 14, 2018 alitembelea, kukagua na kupokea miradi mbalimbali ya Elimu ikiwa ni pamoja na kutembelea baadhi ya shule
za Sekondari na kuonge na wanafunzi wa shule hizo.
Wilayani Muleba
Katika siku yake ya kwanza Mkoani
Kagera Prof. Ndalichako alitembelea na kukagua miundombinu ya Chuo cha Ualimu
Katoke Wilayani Muleba ambapo katika chuo hicho ambacho miundombinu yake
imechoka na alihaidi kuwa kitatengewa bajeti ya ukarabati kuanzia bajeti ya
mwaka 2018/2019 ili kikarabatiwe.
Shule ya Sekondari Profesa Joyce
Ndalichako, Prof. Ndalichako pia alifika katika shule hiyo iliyopewa jina lake
ili kujionea ujenzi wa shule ambayo fedha zake zilitolewa na Serikali, Katika
Shule hiyo Prof. Ndalichako aliridhika na viwango vya ujenzi wa shule hiyo na
kuwapongeza wananchi kushirikiana na Serikali katika kujenga Shule hiyo.
Prof. Ndalichako aliwahasa
wanafunzi kujitahidi katika masomo yao ili wasimwangushe kwani shule hiyo
inaitwa jina lake. Pia alihaidi kutoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya kujenga
Maabara na shilingi milioni 3 kwajili ya kununulia vitabu ili wanafunzi wa
shule hiyo waweze kupata elimu stahiki.
Shule ya Sekondari Prof. Anna
Tibaijuka Muleba mjini, katika ziara yake pia Prof. Ndalichako pia lipata wasaa
wa kuitembelea Shule hiyo ambayo bado ina changamoto ya miundombinu kama
madarasa pamoja samani za viti na meza kwa ajili ya wanafunzi .
Agizo; Baada ya kuona msongamano wa wanafunzi katika
shule hiyo Prof. Ndalichako alitoa Agizo kwa Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya
Nchini kuacha tabia ya kudahili wanafaunzi
juu ya uwezo wa miundombinu katika shule husika. Maafisa Elimu Mikoa na
Wilaya popote nitakapokuta wamedahili watoto kuzidi uwezo wa miundombinu
iliyopo watawajibika wao wenyewe, Alisistiza Prof. Ndalichako.
Prof. Ndalichako alisema kuwa ni
ajabu kuona shule haina madarasa ya kutosha alafu Maafisa Elimu wanawapeleka
wanafunzi wengi katika shule hiyo ambayo haiwezi kuwamudu wanafunzi hao kwa
wakati mmoja. Katika hatua nyingine Prof. Ndalichako alihaidi kutoa mabati 100 ili kumalizia chumba cha darasa
ambalo ujenzi wake unaendelea.
Wilayani Missenyi
Siku hiyo hiyo akiwa Wilayani
Missenyi Prof. Ndalichako alitembelea Chuo cha Maendelea ya Wananchi Gera na
kujionea ukarabati wa Chuo hicho ambapo Serikali ilitoa Shilingi Milioni 75 ili
kukarabati baadhi ya majengo. Prof. Ndalichako hakuridhishwa na kiwango cha
ukarabati uliofanywa na VETA Kagera
katika chuo hicho kwani haundani na thamani ya fedha iliyotolewa.
Waziri Ndalichako aliwakemea VETA
nchini kuwa wamekuwa wakifanya kazi zao
chini ya kiwango na alisema kuwa atatuma ukaguzi maalum katika Chuo hicho ili
kukagua kazi iliyofanyika na kama ikigundulika kuwa kuna uchakachuzi VETA Kagera watalazimika kukiarabati chuo hicho
kwa gharama zao wenyewe, pia ukaguzi huo maalum utapitia na shughuli zao za
kawaida kwani ilionekana kuwa wamekuwa wakifanya madudu.
Post a Comment