Na:
Sylvester Raphael
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Lameck Nchemba
azindua rasmi zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa Mkoani Kagera katika
Kijiji cha Kasindaga Kata Kabitembe Wilayani Muleba leo Februari 16, 2018.
Katika uzinduzi huo Waziri
Mwigulu aliwasisitiza wananchi kuhakikisha kila mmoja kuanzia umri wa miaka 18 nakuendelea
kujiandikisha au kutambuliwa na
kusajiliwa kwaajili ya kupata kitambulisho cha Taifa ambacho ni muhimu sana kwa
kila Mtanzania kwa maisha ya kila siku.
Waziri Mwigulu alisema kuwa
Kitambulisho cha Taifa ni muhimu sana kwa masuala ya kiusalama ambapo kila
mwananchi atatambuliwa, Wakimbizi wote watatambuliwa na wale wote wanaotoa
huduma za kiubalozi watatambuliwa na hakuna Mtanzania ambaye anatakiwa kubaki
bila kutambuliwa.
Pia Waziri Mwigulu amewaasa
wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa na wivu wa uzalendo na nchi yao na mkoa wao pia
kwa kutoa taarifa sahihi kwa wasio raia
wa Tanzania kwa kuwa Kagera kuna vivutio
vingi na
unapakana na nchi nyingi jambo ambalo linawavutia watu au wahamiaji
haramu kuingia nchi jirani.
“ Katika Mahabusu za Mkoa wa
Kagera kuna waharifu wenye kesi za uharifu wa kikatili kuliko mahabusu za mikoa
mingine lakini ukichunguza kwa undani utagundua wahalifu hao siyo Watanzania
bali ni kutoka nchi za jirani ambapo hawana huruka za Kitanzania bali ukatili
tu,” Alitoa mfano Waziri Mwigulu.
Katika Hatua nyingine Waziri
Mwigulu alimwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro kutumia vyombo
vyake vyote vya uchunguzi kuhakikisha
anachunguza mauaji ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini
(Akitolea mfano wa Kijana aliyeuawa Kinondoni wa chama cha CHADEMA) na baada ya
uchunguzi Jeshi hilo litoe taarifa kwa wananchi ili kujua chanzo cha mauaji
hayo.
Kwaniaba ya Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji Hamelore M. Manyanga ambaye ni Kamishna wa Huduma za Sheria katika
uzinduzi huo alitoa rai kwa wananchi kutoa taarifa sahihi wakati zoezi la
utambuzi na usajili wa Vitambulisho vya
Taifa likiendelea. Pia aliwaasa watendaji kuhakikisha wanajiepusha na vitendo
vya rushwa katika zoezi hilo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuli kwa
atakayebainika.
Aidha, Bw. Alphonce Malibicha
Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vitambulisho vya Taifa kwaniaba ya Mkurugenzi
Mkuu wa NIDA alisema kuwa wananchi wanaotakiwa kusajiliwa ni umri kuanzia miaka
18 na kuendelea na raia wa Tanzania .
Pia alisema kuwa uandikishaji unaendelea
katika Mikoa 19 sasa Tanzania Bara na Kagera sasa imeongezeka baada ya
kufanyika uzinduzi rasmi.Bw. Malibicha alizitaja faida za
Vitambulisho vya Taifa kuwa ni pamoja na huduma mbalimbali za kijamii,
Vitambulisho vya Taifa vitatumika katika kusajili Makampuni ambapo mmiliki
taarifa zake lazima zionekane kwenye kitambulisho, Vitatumika wakati wa kupata
Hati ya kusafiria, Vitatumika katika mifuko ya Hifadhi za jamii katika kutoa
huduma za mafao kwa wananchama wake pia na kubaini Wahamiaji Haramu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja
Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu katika uzinduzi huo alitoa maagizo kwa
Watendaji wa ngazi zote kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kufanikisha zoezi la
uandikishaji kwa kusimamia zoezi zima
hasa Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya chini ya Wenyeviti wake Wakuu wa
Wilaya.
Aidha, Mkuu wa Mkoa Kijuu alitoa
wito kwa watendaji kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika zoezi hilo kwani
wakibainika hatua kali zitachukuliwa mara moja. Pia aliwaasa wananchi
kuhakikisha wahudhuria kujiandikisha kwa muda watakaopewa na wasisubiri muda wa
mwisho na kusababisha msongamano.
Mwisho Mh. Kijuu aliwaomba
viongozi wa dini kuwahamasisha waamini wao kujiandikisha kila mmoja. Pia
alisistiza kuwa zoezi la uandikishaji lisichukuliwe kidini wala kisiasa kwa
kuwapotosha wananchi na mwisho wake baadhi yao wakabaki bila kujisajili na
kupata Vitambulisho vya Taifa.
Post a Comment