Na:
Sylvester Raphael
Serikali katika Mkao wa Kagera yapunguza migogoro ya ardhi
kwa kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu Tano changamoto kubwa iliyobaki ni kupangilia miji na kuzuia ujenzi
holela katika Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba.
Hayo yamesemwa leo Februari 19,
2018 na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Wiliamu Lukuvi mara baada ya
kuwasili Mkoani Kagera kwa ziara ya siku nne katika Wilaya za Bukoba
(Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Manispaa ya Bukoa), Karagwe, Kyerwa na
Ngara.
Mara baada ya kupokea taarifa ya Mkoa ihusuyo Wizara
yake kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Waziri Lukuvi aliwapongeza watendaji katika mkoa kuendelea kutatua migogoro ya
ardhi na kutozalisha migogoro mipya bali migogoro iliyopo ni ile iliyozalishwa
kipindi cha nyuma kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano haijaingia madarakani.
Waziri Lukuvi alisema kuwa
Serikali iliamua kurasimisha maeneo ambayo tayari yalikuwa yamejengwa holela
ili kupangilia miji lakini kuanzia sasa wananchi hawaruhusiwi kujenga holela na
Watendaji wa Halmashauri hasa Maafisa wa Mipango Miji wanatakiwa kutoa Ramani
za kila eneo kwa Watendaji wa Mitaa ili kuzuia ujengaji holela bila vibali vya
ujezni vya Halmashauri husika.
“Kulikuwa na ucheleweshaji wa
vibali vya ujenzi katika Halmashauri lakini kwa sasa Serikali imeamua kutoa
kipengele cha vibali kupitishwa na Mabaraza ya Madiwani ili kuharakisha vibali
vya ujenzi kutoka haraka kwa mwananchi anayetaka kujenga nyumba yake,”
Alisistiza Waziri Lukuvi.
Katika kusisitiza suala hilo
Waziri Lukuvi alisema kuwa Wataalamu wa Ujenzi, Mipango Miji na Mkurugenzi
wanatakiwa kukaa na kupitia maombi ya vibali vya ujenzi na kutoa taarifa katika
vikao vya Mabaraza ya Madiwani. Waziri Lukuvi alisema kuwa tayari Waziri wa
Ofisi ya Rais TAMISEMI amesaini waraka wa kuondoa kifungu hicho ili vibali
vipitishwe na Wataalam.
Katika hatua nyingine Waziri
Lukuvi alitoa rai kwa wananchi wa Kagera kuwa kuna wananchi mashamba yao yapo
katika miji lakini hawataki yapimwe ambapo alitoa karipio kali kwa wananchi hao
na kusema kuwa mpangaji wa ardhi ni Halmashauri, kama Serikali ikihitaji ardhi
hiyo itamfidia mwananchi husika na kutumia ardhi hiyo kama ilivyopangwa
.
Pamoja na kutatua migogoro ya
ardhi iliyoshindikana katikaHalmashauri za Wilaya zilizotajwa hapo juu Waziri
Lukuvi pia atafuatilia suala la ulipaji wa kodi za ardhi katika maeneo
atakayotembelea ili kona jinsi kodi hizo zinavyokusanywa na kuwahamasisha
wananchi kulipa kodi hizo na Halmashauri kuchukua wajibu kikamilifu katika
ukusanyaji.
Ikumbukwe kuwa katika Mkoa wa
Kagera vimepimwa viwanja 2,897 kuanzia mwaka 2016 hadi kufikia sasa, aidha
Halmashauri za Wilaya zote nane katika Mkoa wa Kagera zinaendelea na upimaji na
kutao hati za viwanja.
Post a Comment