Home
»
News
» MAAFISA HABARI NA TEHAMA WANOLEWA KUZIBORESHA TOVUTI ZA MIKOA NA HALMASAHURI ILI KUWA KITOVU CHA HABARI KWA WANANCHI
Na: Sylvester Raphael
Serikali kupitia Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Mradi
wa kuboresha Mifumo ya Serikali PS3 waendesha mafunzo ya siku nne juu ya namna
bora ya uandishi wa habari za Tovuti za Serikali kwa Maafisa Habari na Maafisa
Tehama wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara.
Kutokana na umuhimu wa Tovuti
za Serikali hasa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa nchini kuwa chanzo kikuu
cha habari kwa wananchi Serikali kwa kushirikiana na Mradi wa Maboresho ya
Mifumo ya Serikali PS3 waliona kuna umuhimu wa kuendesha mafunzo juu ya
uandishi bora wa habari katika Tovuti za Mikoa na Halmashauri ili wananchi wapate habari muhimu na zenye
uhakika juu ya maendeleo yao.
Kwakuwa siyo Mikoa yote na
Halmashauri zote nchini zina Maafisa Habari na kazi za Habari zinafanywa na
baadhi ya watu kama Maafisa Tehama, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mradi wa
kuboresha Mifumo ya Serikali PS3 wameona kuna umuhimu wa Maafisa hao kupitishwa
katika mafunzo ya namna bora ya uandishi wa habari za Tovuti kwa wananchi ili
kuwa na uelewa wa pamoja na aina moja ya uandishi (House Style)
Katika Mafunzo hayo mada
mbalimbali zihusuzo Uandishi wa Habari zinawasilishwa na wataalamu waliobobea
katika mambo ya habari na uandishi wa habari pia ambapo mada hizo ni pamoja na
Malengo ya Mwongoz wa Tovuti, Sheria na
Maadili ya Habari, Upigaji wa Picha za Kidijitali, Mbinu za Mahojiano, Uandishi
wa Aya, Habari katika mfumo wa 5Ws + H (Piramidi iliyogeuka).
Mafunzo ya namna bora ya
uandishi wa habari za Tovuti za Serikali yanaendeshwa katika makundi ya mikoa mbalimbali
ambapo mikoa ya Geita, Tabora Kigoma na Kagera mafunzo hayo yanafanyika katika
Mkoa wa Kagera Bukoba Hotel Manispaa ya Bukoba aidha, mafunzo hayo yalianza
Februari 19 na yanatarajia kukamilika Februari 22, 2018.
Matarajio ya Serikali baada
ya mafunzo hayo ni kuona Tovuti za Serikali zinakuwa kitovu cha habari kwa
wananchi na si ilimradi habari tu bali habari zenye weledi, ukweli, uhakika na
kuisemea Serikali inafanya nini katika kuwaletea wananchi maendeleo. Pia katika
Tovuti hizo kuwa na taarifa muhimu mbalimbali zinazohusu taasisi husika mfano
Mkoa au Halmashauri husika.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Related Posts
- KAGERA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KUENDELEA KUJIIMARISHA KUWALINDA RAIA NA MALI ZAO25 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Vyombo ya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera vyafanya mazoezi ya ...Read more »
- MBIO ZA MWENGE WA UHURU KATIKA WILAYA ZA KARAGWE NA NGARA PIA HITIMISHO WILAYANI BIHARAMULO MKOANI KAGERA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mwenge wa Uhuru waendelea kuchanja mbuga Mkoani Kagera kwa ku...Read more »
- MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI KAGERA NA KUANZA UZINDUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YABILIONI 1216 Apr 20180
Na: Sylvester Rapahel Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo April 8, 2018 Mkoani Kagera na...Read more »
- TIMU YA WATAALAM WA UJENZI KUTOKA NCHINI CHINA YAKAGUA ENEO LA UJENZI WA CHUO CHA VETA KAGERA ILI KUANZA UJENZI MARA MOJA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Serikali ya Watu wa China yatuma timu ya Wataalam wa Usanif...Read more »
- MKOA WA KAGERA WAVUKA LENGO KATIKA UNDIKISHAJI WA WANAFUNZI AWALI NA DARASA LA KWANZA MWAKA 201816 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mkoa wa Kagera wavuka lengo la uandikishaji wa Wananfunzi katika madarasa...Read more »
- MKUU WA MKOA KAGERA AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUFIKISHWA OFISINI KWAKE AKIWA NA PINGU MIKONONI BAADA YA KUITIA SERIKALI HASARA08 Mar 20180
Na Sylvester Raphael Mkuu wa Mkoa wa Kagera aagiza Mkandarasi wa Kampun...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.