Na
Sylvester Raphael
Mkuu wa Mkoa wa Kagera
aagiza Mkandarasi wa Kampuni ya MECCO
aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa barabara
zenye thamani ya shilingi bilioni saba na kukataa kusaini mkataba wa kuanza ujenzi katika Halmashauri ya Manispaa
ya Bukoba kukamatwa na kufikishwa Ofisini kwake akiwa na pingu mikononi ili
kutoa sababu za kuitia Serikali hasara.
Mhe. Meja Jenerali Mstaafu
Salum M. Kijuu alitoa agizo hilo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa kwenye kikao cha
Bodi ya Barabara kilichofanyika Mkoani Kagera Machi 8, 2018 ambapo katika
kuwasilisha hoja Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Chief Karumuna kumuomba Mkuu Mkoa kumchukulia hatua
Mkandarasi huyo baada ya kugoma kusaini mkataba wakati alishinda zabuni ya
ujenzi wa barabara hizo.
Chief Karumuna alisema kuwa
Manispaa ya Bukoba imepata hasara baada ya Mkandarasi kukataa kusaini mkataba
wa kuanza ujenzi wa barabara zenye thamani ya shilingi bilioni saba na zabuni
kutangazwa tena upya, pia alisistiza kuwa fedha hizo zilitolewa na Benki ya
Dunia na utekelezaji wa miradi yake ni wa kipindi maalumu kwa hiyo Mkandarasi
huyo amechelewesha muda wa utekelezaji.
Katika kikao hicho ambacho
Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti aliwasistiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini
TARURA Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanatengeneza barabara za mipakani ili
kuimarsha ulinzi na usalaama wa mkoa na na chi kwa ujmla. Barabara hizo ni
Bubale-Missenyi Runch- Kakunyu Kilomita
32.5, Bubale – Kamwema Kilomita 17.8
Wilayani missenyi na barabara ya Nyabishenge-Nyakanoni-Ibanda Game
Reserve kilomita 15 Wilayani Kyerwa.
Vilevile Meneja wa Wakala wa
Umeme na Ufundi (TEMESA) Mkoa wa Kagera ameagizwa na kikao hicho kusitisha mara
moja tozo ya shilingi 80,000/= ya ukaguzi wa magari ya Serikali pale
yanapotakiwa kukaguliwa ili yakatengenezwe baada ya wajumbe kuwasilisha sheria
kikaoni inayoelekeza kuwa magari ya Serikali yanatakiwa kukaguliwa bure. Hadi
Mkuu wa mkoa atakapopata walaka unaoruhusu kutoza magari ya Serikali.
Mkoa wa Kagera unahudumia
barabara zenye mtandao wenye jumla ya kilomita 7,505.42 kati ya hizo, kilometa
675.46 ni barabara za lami, kilometa 2,791.56 barabara za changarawe na
kilometa 4,038.96 zikiwa in barabara za udongo.
Mkoa wa Kagera kwa mwaka wa
fedha 2017/18 uliidhinishiwa shilingi Bilioni 10,710.05 kwajili ya matengenezo
ya kazi za barabara na ujenzi wa madaraja. Pia mkoa umeidhinishiwa shilingi
bilioni 14,180.937 kwa ajili ya
matengenezo ya Barabara Kuu na Barabara za Mkoa kwa mwaka wa fedha 2017/18
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa wa Kagera
amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka kumkamata na kumpeleka
ofisini kwake kijana anayemtesa mama yake mzazi kwa kutaka kumnyanganya shamba
lake na mama huyo ameshinda kijana huyo mara mbili Mahakamani.
“Mtafute kijana huyo na kumleta kwangu nijue ana matatizo gani ili
tumsaidie maana atamuua mama yake, hana uchungu na mama yake mzazi. Mama
huyoaliwasilisha kilio chake katika mkutano wa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya
Makazi Mhe. Lukuvi Wilayani Karagwe lakini kijana huyo bado anaendelea
kumsumbua mama yake mzazi.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Kijuu.
Post a Comment