Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: KUTUMIA VIZIBITI MIMBA,UTOAJI MIMBA HIVYO VINACHANGIA KUTOA UHAI WA MWANADAMU
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Jamii imetakiwa kutambua umuhimu wa uhai wa mwanadamu tangu inapotungwa mimba hadi kuzaliwa kwa   kuepuka baadhi ya vitu vinavyosababish...

Jamii imetakiwa kutambua umuhimu wa uhai wa mwanadamu tangu inapotungwa mimba hadi kuzaliwa kwa  kuepuka baadhi ya vitu vinavyosababisha kuondoa uhai wa mwanadamu ikiwemo madawa ya kupanga uzazi utoaji mimba,na magonjwa ya zinaa.


Hayo yamesema na Mwezeshaji  Emili Agamu katika  semina juu ya utetezi wa uhai iliyofanyika katika makao makuu ya Jimbo Katholiki la Kayanga ikihusisha wajumbe kutoka Dekania ya Bugene ambayo inaundwa na parokia za Ndorage,Bugene, na Parokia ya Mtakatifu George.

Agamu amesema kuwa mwanzo wa uhai wa mwanadamu uko mikononi mwa Mungu na anayeamua kuondoa uhai huo ni Mungu pekee lakini katika dunia ya sasa binadamu wamechangia katika kuondoa uhai wa binadamu wenzao  kwa kutumia madawa ya kuzuia mimba yaani Vidhibiti mimba,magonjwa ya zinaa na sababu nyinginezo ambapo amesema kuwa hayo yote ni chukizo kwa Mungu na sio maelekezo ya Kanisa katholiki.

Amesema kuwa sababu nyingine ya kutoa uhai wa mwanadamu ambayo kwa sasa imeshamili ni utoaji wa mimba ambapo wanaofanya hivyo hudai kuwa wanapanga uzazi,hali ngumu ya maisha na sababu nyingine kama za kubakwa .

Agamu ametaja   madhara mbalimbali ya kutoa mimba  yakiwemo ya  kimwili, kiakili na kiroho ambapo amezitaka familia kuachana na vitendo hivyo viovu kwani kwa kufanya hivyo unakuwa umeondoa uhai wa binadamu na ukizingatia kuwa mwenye uwezo wa kuondoa uhai ni Mungu pekee.

Kwa upande wake Askofu Almachius Vicent Rweyongeza amesema kuwa wakristo wengi sasa wanaharibu miili yao kwa namna mbalimbali ambapo amewataka kumrudia Mungu na kuachana na anasa za hapa duniani.

Semina hii ya utetezi wa uhai itaendeshwa kwa Dekania nne ambazo ziko ndani ya Jimbo hili la Kayanga.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top