Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: UTAPELI KARAGWE WANANCHI WATAHADHARISHWA WAWE MAKINI NA WATU WASIOWAFAHAMU
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi kata ya Kayanga Wilayani Karagwe wametaadhalishwa kuwa makini   katika maeneo wanakopita baada ya utapeli   ambao umeone...




Wananchi kata ya Kayanga Wilayani Karagwe wametaadhalishwa kuwa makini  katika maeneo wanakopita baada ya utapeli  ambao umeonekana kuibuka na kuwaumiza baadhi ya wafanyabiashara  na watu wengine.



Hayo yamebabinishwa na mwenyekiti wa KATOMA RUZINGA  Amos Kahwa  katika mahojiano maalum ambapo ametaja suala la utapeli kuwa tatizo kubwa kwenye kata hiyo.



Amos amesema kuwa katika kipindi kifupi cha mwezi machi matukio kadhaa ya utapeli yamekuwa yakiripotiwa hususan katika maduka ya Mpesa huku akitaja vijana ambao wengi wao ni wanafunzi wa ngazi ya sekondari kuhusika kwa wingi katika utapeli huo.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi katika kata ya kayanga na wilaya ya karagwe kwa ujumla kuwa makini na mali zao na watoe taarifa katika ofisi za kata na jeshi la polisi katika kuhakikisha kuwa wahalifu hao wanapatikana.


Sambamba na hayo ametoa rai kwa vijana wasiokuwa na shughuli maalum katika kata yake kurudi vijijini mara moja kabla hawajakamatwa na kutiwa nguvuni na jeshi la polisi.

Katika hatua nyingine amewataka wamiliki wa nyumba za kukodisha kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa juu ya kaya zao kwa kutoa taarifa muhimu za wapangaji wao kwa mwenyekiti wa mtaa husika.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top