Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WATAKIWA KUWATUNZA WAJAWAZITO NA WATOTO KUANZIA UMRI SUFURI HADI MIAKA SITA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
JAMII mkoani KAGERA  imeshauriwa kuwatunza wajawazito na watoto kuanzia   umri sifuri hadi miaka sita ili kuwajengea ubongo changamfu kuanz...
JAMII mkoani KAGERA  imeshauriwa kuwatunza wajawazito na watoto kuanzia   umri sifuri hadi miaka sita ili kuwajengea ubongo changamfu kuanzia wanapokuwa katika umri mdogo.

Kauli imetolewa  na mkurugenzi wa shirika la  (Mapec) la wilayani  Missenyi mkoani Kagera   Dr GEORGE BUBERWA   katika Semina ya makuzi ya mtoto iliyozaminiwa na USAID, Pact Hilton Fonra Foudation .

Dr BUBERWA   amesema  kuwa ili kuzalisha mtoto atakae kuwa bora kuna kila sababu ya kuwekeza katika ubongo ili kutayarisha kizazi ambacho kitakuwa na maamuzi yaliyo bora na sio ilimradi kizazi.

Amesema  kuwa ubongo ni kiungo muhimu sana katika kiungo cha mwanadamu hivyo usipo jengewa mazingira mazuri toka udogoni kuna hatali ya kulikosa Taifa yenye fikra. mpya.

Amebainisha  kuwa Kuna vitu muhimu vyakuzingatia katika makuzi ya mtoto ambayo ni kuzingatia lishe kuanzia kwa mama anapokuwa amepata ujauzito kuanzia siku ya kwanza anapaswa kutunzwa na kupendwa ili mtoto atakaezaliwa awe  na ubongo unaofanya kazi vizuri.

Amefafanua ili  kuondoa dhana ya kuzalisha watoto wasio na fikra mpya kuna kila sababu ya wazazi na jamii, Serikali kushiliki katika kuwalea watoto kwa kuwapenda, kucheza nao, pamoja na kuwapatia lishe iliyo bora nasio kuwaterekeza .

Aidha, amesema kuwa Kutokana na utafiti ulifanywa na wanasayansi inaonekana kuwa ubongo wa mtoto unapo tunzwa vizuri kuanzia umri sifuri hadi miaka sita kuna asilimia kubwa ya kupunguza uhalifu nchini, maana mtoto aliepata lishe ya kutosha pamoja na kutunzwa vyema anakuwa naufahamu mkubwa kuanzia anapo kuwa katika shule za awali mpaka anapofikia elimu ya juu.

Kwa upande wake ofisa ustawi wa jamii  wa Halmashauri ya  Wilaya Missenyi ANORD NKONGOKI amesema  wanaume wamekuwa changamoto kwa akina mama wajawazito pamoja na watoto khali inayopelekea wanaume wengi kutelekeza familia na watoto kushindwa kupata makuzi mazuri.

Kwa mujibu wa ofisa huyo takwimu zinaonyesha kuwa Mpaka sasa kuna kesi 55 zinazotokana  na wanaume kuoa wanawake wengi na kushindwa kuwahudumia, akinamama wajawazito kupigwa pasipo huruma,akina mama kutelekezwa na watoto wachanga ambapo amebainisha kuwa swala hilo linafanyiwa kazi na halmashauri hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top