Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI KAGERA NA KUANZA UZINDUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YABILIONI 12
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Na: Sylvester Rapahel Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo April 8, 2018 Mkoani Kagera na Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Sal...


Na: Sylvester Rapahel




Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo April 8, 2018 Mkoani Kagera na Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel katika Kijiji cha Nyakabango mpakani mwa Geita na Kagera ambapo katika Mkoa wa Kagera Mwenge wa Uhuru utapitia miradi ya maendeleo 65 yenye thamani ya shilingi bilioni 12,385,330,354.



Katika miradi hiyo 65 Mwenge wa Uhuru utazindua miradi 33, utakagua miradi 19, utaweka mawe ya msingi katika miradi 13 aidha,  mchanganuo wa gharama za miradi hiyo 65 itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni kama ifuatavyo, Serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi bilioni 5,817,795,968 sawa na asilimia 47%.


Halmashauri za Wilaya zimechangia  kiasi cha shilingi 671,940,497 sawa na asilimia 6%. Aidha wananchi wamechangia shilingi bilioni 2,181,496,962 sawa na asilimia 17%.  Wahisani wamechangia shilingi bilioni 3,714,096,927 sawa na asilimia 30%. 



Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2018 umebeba kaulimbiu isemayo “Elimu ni ufunguo wa Maisha; Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu.” Kauli mbiu hii inawahamasisha wananchi hususani wa Mkoa wa Kagera kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto shule ili mkoa wetu na Taifa kwa ujumla lipate wataalam wa kutosha katika kada mbalimbali za kitaaluma na hapo taifa letu litapiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kuwatumia wataalamu wetu wa ndani.


Pamoja na Kauli Mbiu tajwa hapo juu Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wetu zitaendelea kuwahamasisha wananchi kuhusu Mapambano dhidi ya Rushwa, Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Mapambano dhidi ya Matumizi ya Dawa za Kulevya na Mapambano dhidi ya Malaria.


Mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Luyango na Mwenge wa Uhuru ukaanza mara moja mbio zake wilayani humo za kukagua miradi ya maendeleo.


Akitoa ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kiongozi wa Mbio hizo Charle Francis Kabeho katika eneo la Nyakabango aliwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii masomo ya Sayansi kwani Serikali imefanya kazi yake ya kujenga shule na vyumba vya mahabara na kuweka vifaa vya kutoasha katika maabara hizo



About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top