Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MBIO ZA MWENGE WA UHURU KATIKA WILAYA ZA KARAGWE NA NGARA PIA HITIMISHO WILAYANI BIHARAMULO MKOANI KAGERA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Na: Sylvester Raphael Mwenge wa Uhuru waendelea kuchanja mbuga Mkoani Kagera kwa kuendelea kuzindua, kuweka mawe ya msingi...




Na: Sylvester Raphael


Mwenge wa Uhuru waendelea kuchanja mbuga Mkoani Kagera kwa kuendelea kuzindua, kuweka mawe ya msingi, kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya za Karagwe na Ngara.



Katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa Wilayani humo tarehe 13 Aprili, 2018 ambapo jumla ya miradi 12 ilipitiwa na Mwenge wa Uhuru na kukagua, kuizindua, kuweka mawe ya msingi na kuona uendelevu wa miradi iliyopitiwa na Mwenge huo mwaka jana 2017



Katika Miradi hiyo 12 iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru Wilayani Karagwe wananchi walichangia kiasi cha shilingi 1,339,482,000/=, Halmashauri shilingi 28,085,600/=, Wahisani shilingi 789, 234,132/=, na Serikali Kuu shilingi 766,578,211/= ambapo thamani ya miradi yote jumla ni shilingi 3,175,124,660/=.



Mwenge wa Uhuru umeendelea na mbio zake leo Aprili 14, 2018 Wilayani Ngara mara baada ya kukabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara Michael Mtenjele kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka.


Ukiwa Wilayani Ngara Mwenge wa Uhuru umeweza kuipita miradi ya maendeleo yenye thanmani ya shilingi bilioni 207,026,400/= katika Sekta za Kilimo, Elimu, Huduma za Jamii kama Afya na Maji, pamoja na miundombinu ambayo ni barabara.

Ukiwa Wilayani Biharamulo April 15, 2018 Mwenge wa Uhuru ulipitia miradi ya maendeleo ipatayo sita na yenye thamani ya shilingi milioni 917,976,109/=

Akitoa ujumbe wa Mbio za Mwenge Wilayani humo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles Kabeho aliwasisitiza wananchi kuwekeza katika Elimu ili kuinua uchumi wa nchi yetu. Aidha, aliwasisitiza wananchi kuhamasika katika shughuli za kiuchumi ili kujiletea maendeleo na kuachana na shughuli zisizokuwa na tija kama kujihusisha na kilimo cha bangi ambayo ni madawa ya kulevya.



Mwenge wa Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake mkoani Kagera utakabidhiwa Mkoani Kigoma tarehe 16 April, 2018 ili kuendelea na mbio zake mkoani humo.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top