Unknown Unknown Author
Title: WALIOMBAKA BINTI WA MIAKA 21 NA KUSAMBAZA PICHA WAFIKISHWA MAHAKAMANI MOROGOGORO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  Watu   6 wanaodaiwa  kumbaka   Binti  wa  miaka 21  wilayani  Mvomero  mkoani  Morogoro  wamefikishwa  mahakamani  na  kusomewa  mash...

 Watu   6 wanaodaiwa  kumbaka   Binti  wa  miaka 21  wilayani  Mvomero  mkoani  Morogoro  wamefikishwa  mahakamani  na  kusomewa  mashtaka  yanayowakabili  na  wamerudishwa  rumande mpaka juni mosi mwaka  huu.
Watuhumiwa  hao  waliotajwa  kwa  majina  ya  Zuberi  Thabiti  miaka (30)mkazi  wa Mbalali  mkoani  Mbeya  ambaye  ndiye  mbakaji,na  Idd  Adamu  miaka  32 ambaye  anatuhumiwa  kurekodi  video  ya  ubakaji  ni  mkazi  wa  Njombe
Kesi  hiyo  inayosimamiwa  na  waendesha  mashtaka  watatu  wa  serikali  ambao  ni  Gloria  Rwakibala ,Edigar  Bantulaki  na  Kalistus  Kapinga .
Imeelezwa  kuwa  tukio  hilo lilitendeka  April  27 saa  moja  usiku  katika  nyumba  ya  Kulala  wageni  ya  Titii   ya  Tarafa  ya  Dakawa   wilaya  ya  Mvomero  Mkoani  Morogoro
 Edgar Bantulaki, mwendesha mashataka amedai kuwa, washtakiwa hao wamefanya kosa hilo chini ya kifungu cha sheria namba14 (1) (b) na 2 (b) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.

Bantulaki amewataja washtakiwa wengine kuwa ni pamoja na mshtakiwa namba 1 na 2 na Rajabu Salehe, (30), Ramadhani Ally (26), Muhsin Ng’ahy (36), John Peter (24) wote wakiwa ni wakazi wa Wami, Dakawa wilayani Mvomero.

 Watuhumiwa  hao  wamenyimwa  dhamana  kutokana  na  tukio  hilo  kuvuta  hisia  kubwa  za  watu  wengi  Tanzania  nzima.

Aliyeshikwa  kichwani  na  askari  ni  Idd  Adamu  (32)mkazi  wa  Njombe  anayetuhumiwa  kurekodi  video  ya  ubakaji  na  huyo  mwingine  mwenye  jackti  nyeusi  ni  Zuberi  Thabiti  (30) mkazi  wa  Mbalali -mkoani  Mbeya  anayetuhumiwa  kubaka  binti  huyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top