Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: KAGERA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KUENDELEA KUJIIMARISHA KUWALINDA RAIA NA MALI ZAO
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Na: Sylvester Raphael Vyombo ya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera vyafanya mazoezi ya pamoja ili kijiweka tayari na kushiriki...


Na: Sylvester Raphael




Vyombo ya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera vyafanya mazoezi ya pamoja ili kijiweka tayari na kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza jukumu moja kuu la kuwalinda raia na mali zao.


Mazoezi hayo yaliyofanyika katika Manispaa ya Bukoba Aprili 25, 2018 yameyashirikisha Majeshi ya Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto, Jeshi la Akiba na Jeshi la Wananchi Tanzania.


Akiongea na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Augustino Olomi mara baada ya kuhitimisha mazoezi hayo katika Viwanja vya Gymkhana alisema kuwa ni mazoezi ya kawaida kwa Majeshina kitaalam yanaitwa (Route Match)



“Mkoa wa Kagera tumekuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi haya kila Jumamosi ya kila wiki kwa kushirikiana na wananchi lakini leo wananchi wapo kwenye shughuli zao  za uzalishaji, Majeshi kama unavyoyaona tumeshirikiana kufanya mazoezi ya pamoja kwani sote jukumu letu ni kulinda raia na malizao,” Alifafanua Kamanda Olomi



Aliongeza Kamanda Olomi kuwa Majeshi yakifanya mazoezi ya pamoja wanakuwa na utayari wa pamoja kupambana na vitendo ambavyo vinaweza kuhatarisha usalama wa raia na mali zao lakini pia na Askari katika mazoezi haya wanafahamiana kwa karibu jambo linaloleta ushirikiano mzuri katika kazi.



Aidha, Kamanda Olomi alitumia nafasi hiyo kuwatahadharisha wale wote wanaopanga kundamana au kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani siku ya maadhimisho ya Muungano tarehe 26 Aprili, 2018 kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera limejipanga vizuri kushughulika nao kikamilifu.


Kamanda Olomi alisisitiza kuwa mwananchi yeyote asidanganyike kwa kushawishiwa kuandamana na aliwataka wananchi hao kuendelea na shughuli zao za kawaida za baishara, kilimo au kutumia siku hiyo kupumzika kuliko kujihusisha kwenye vitendo ambavyo vinaweza kuwaletea matatizo.


Mazoezi ya pamoja ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera yalianzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kupitia katikati ya mji wa Bukoba kuelekea Kashai na yamehitimishwa katika Viwanja vya Gymkhana karibu na Bukoba Club.


Wito kwa wananchi wote hususani Manispaa ya Bukoba mnakaribishwa kila Jumamosi ya kila wiki kujumuika pamoja watumishi  kufanya mazoezi ya pamoja  kwaajili kuimarisha miili yetu, mazoezi hayo huanzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa saa 12:00 Asubuhi na kumalizikia  katika viwanja vya Gymkhana saa 3:00 asubuhi.




About Author

Advertisement

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top