Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: UONGOZI WA KAMPUNI YA STAMIGOLD WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA KAGERA KUJITAMBULISHA NA KUMWELEZA SHUGHULI ZAO
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
  Uongozi wa   Kampuni ya STAMIGOLD   ukiongozwa na Meneja Mkuu Mhandisi Denice Sebugwao walifika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera   ta...
 
Uongozi wa  Kampuni ya STAMIGOLD  ukiongozwa na Meneja Mkuu Mhandisi Denice Sebugwao walifika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera  tarehe 3 Mei, 2016 kujitambulisha na kumsalimia Mkuu wa Mkoa wa Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu.


Uongozi huo wa Kampuni ya STAMIGOLD ukiongea na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu walimpongeza kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mkuu wa mkoa wa Kagera na kumweleza shughuli wanazozifanya katika Kampuni yao iliyopo Wilayani Biharamulo.
 
Mhandisi Sebugwao alimweleza Mhe. Kijuu kuwa Kampuni ya STAMIGOLD iliuchukua mgodi uliokuwa ukijulikana kama TULAWAKA mara baada ya kumaliza uchimbaji na Serikali kuuchukua mgodi huo na kuunda  Kampuni ya STAMIGOLD na kuendelea na uchimbaji kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia mwaka 2014.

Mhandisi Sebugwao amesema kuwa tangu waanze uzalishaji tayari wamejipatia Dollar za Kimarekani milioni 37 aidha, Kampuni hiyo tayari imefanya utaratibu wa kuongeza muda kutoka miaka miwili hadi miaka 10 ili kuendelea na uzalishaji zaidi.
 
Mhe. Kijuu alimuuliza Mhandisi Sebugwao kuhusu mahusiano na huduma wanazozitoa kwa jamii mara baada ya kuanza  uzalishaji. Mhandisi Sebugwao alisema wanaisaidia jamii inayowazunguka kwa kujenga barabara, zahati, na vyumba vya madarasa aidha,  kutoa huduma za maji kwa wananchi katika Wilaya ya Biharamulo.


Aidha, matatizo yanayoikumba Kampuni hiyo STAMIGOLD ni kutumia umeme wa jenereta badala ya umeme wa gridi ya taifa, wananchi kuvamia mgodi na kuiba mali, Uharibifu wa misitu kuzunguka mgodi, na wafugaji kuachia mifugo yao katika eneo la mgodi wakati uzalishaji ukiendelea.
 
Baada ya maelezo hayo Mhe. Kijuu aliupongeza uongozi huo kwanza  kwa kuchimba dhahabu wakiwa kama Kampuni ya Wazalendo  wa Kitanzania. Pili aliwataka kuhakikisha wanashirikiana na kikosi cha Jeshi la Wananchi  kilichoko Biharamulo na Jeshi la Polisi kudumisha ulinzi wa mgadi huo.
 
Pia Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu aliushukuru uongozi huo kwa kulipa kodi ambapo hadi Mwezi Machi Kampuni hiyo ilikuwa ilipa Seriaklini bilioni 16 na inategemea kulipa bilioni 8 kukamilisha bilioni 24. Kuhusu matatizo waliomweleza alisema atayashughulikia na alihaidi kuutembela mgodi huo ili kujionea uzalishaji wa dhahabu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top