Wananchi wametakiwa
kujiunga kwenye vikundi
vya vikoba ili
waweze kuinua kipato
chao kwa kununua
hisa na kusaidia
jamii kwa watu
wenye uhitaji kwenye
maeneo yao.
Wito huo
umetolewa na wanakikundi
cha WAPENDANAO cha
kijiji cha Ihembe two
wilayani Karagwe katika
sherehe za kuvunja
sanduku na kuanza
mwaka mpya wa
kununua hisa za
Kikundi hicho.
Kikundi cha
WAPENDANAO kilichoanzishwa
mwaka 2012 kikiwa
na wanachama 8
sasa kiendelea kukua
na kujiwekea malengo
mbalimbali kwa kuanzisha
miradi kadhaa ya
kusaidiana na kusaidia
jamii pia ikiwemo kuwasaidi hata
watoto yatima.
Katika risala
ya kikundi hicho
cha WAPENDANAO wanayo
miradi kadhaa ikiwemo
ufugaji nyuki,mbuzi na
kina utaratibu kwa
kulinda na kuendeleza
nidhamu ndani ya
kikundi hicho.
Risala hiyo
ilibainisha pia msaada
wanaoupata kutoka ulezi
wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri
Tanzania KKKT dayosisi
ya Karagwe.
Mkuu wa
wilaya ya Karagwe
Deodatusi Kinawiro ndiye alikuwa
mgeni rasmi ambapo
amewakilishwa na Katibu
tawala wa wilaya
Mustapha Said amesema
kikundi hicho kina
sifa zote za
kukopesheka hivyo kitaweza
kufikiriwa na serikali.
Hata hivyo
wanakikundi hicho wameomba
ushirikiano na Idara
ya maendeleo iendelee
kuwalea kama ambavyo
inafanya hivi sasa
kwani kuwepo kwao
ni muhimu.

























Post a Comment