Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: TANZANIA HIGHER LEARNING INSTITUTIONS TRADE UNION, UDOM BRANCH-OFFICE OF THE CHAIRMAN
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
MAELEZO YA KINA KUHUSU UFUNDISHAJI WA DIPLOMA YA SAYANSI, HESABU NA TEHAMA 1. Utangulizi Kuanzia Novemba 2014, Chuo Kik...





MAELEZO YA KINA KUHUSU UFUNDISHAJI WA DIPLOMA YA SAYANSI, HESABU NA TEHAMA

1. Utangulizi

Kuanzia Novemba 2014, Chuo Kikuu cha Dodoma kilianza kupokea wanafunzi wa kusomea stashahada maalum ya diploma ya Elimu, Sayansi, Hisabati na Tehama (DE-SMICT). Lengo kubwa la programu hii maalum ni kutimiza azma ya serikali kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la walimu wa sayansi katika shule za sekondari nchini. Serikali iliamua kuwaleta wanafunzi hawa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) badala ya kupeleka kwenye vyuo vya ualimu ikiamini kwamba UDOM kuna miundombinu ya kutosha hasa majengo na rasilimaliwatu ya kutosha kuweza kuhifadhi wanafunzi hao. Menejimenti na jumuiya nzima ya UDOM iliona ni heshima kupewa jukumu hili na kulipokea kwa mikono miwili. Kukubaliwa na kupokelewa jukumu hili UDOM ililazimika kujipanga upya kimkakati, kimfumo pamoja na kufanya mabadiliko kadha wa kadha katika utendaji wake wa kila siku ili kuweza kuhimili jukumu hili kubwa la kitaifa. Mojawapo ya hatua zilizochukuliwa ilikuwa kuunda Kikosi Kazi (Steering Committee- SC) cha kushauri namna ya kukabili jukumu hili.

1.1 Kuundwa Kamati Maalum ya Uratibu (Steering Committee-SC)

Kuundwa kamati ya kuratibu ufundishaji wa wanafunzi hawa (SC) ulionekana kuwa ni muhimu sana kutokana na ukweli kwamba ni lazima kutafuta utaratibu tofauti wa utoaji taaluma kwa vijana. Kamati hiyo iliundwa kwa kuwashirikisha Koleji, Skuli na Idara zinazohusika na masomo ya sayansi, ualimu na TEHAMA.

Kwa msingi huu, Koleji za Elimu, Sayansi asilia na Kumpyuta ndizo zilizohusika katika kuunda kamati hiyo. SC iliyoundwa ilipewa jukumu la kuratibu namna bora ya kushughulikia masuala ya taaluma, malazi, nk. na kupeleka mapendekezo ngazi za juu kwa maana ya Menejimenti ya UDOM na vyombo vya maamuzi ya kitaaluma kama Udhibiti wa Ubora (Quality Assurance) na Seneti ya UDOM (Senate).

Kabla ya kuanza kufundisha, SC ilipendekeza mikakati, mifumo na mabadiliko yaliyokuwa ya msingi ili kukabili swala hili. Changamoto kubwa, ilibainika ni, ufundishaji wa hawa vijana. Masuala mengine yahusuyo malazi na malezi kwa ujumla wake yaliandaliwa ingawa hayakuwa na changamoto kubwa kama suala la

UFUNDISHAJI. Suala la ufundishaji lilihitaji jicho la pekee kwani vijana hawa waliopokelewa ndiyo kwanza wamemaliza kidato cha nne, hivyo bado ni wadogo kwa kiasi fulani na pia hawakupaswa kufundishwa kama wenzao wanaosomea masomo ya shahada na kuendelea. Ifuatayo ni mikakati ya ufundishaji iliyoshauriwa na SC-UDOM ili kuweka mazingira mazuri ya vijana hawa kusoma kwa ufanisi.

1.2 Ugawaji wa Mikondo (Streams)

Kama ilivyobainishwa hapo awali kwamba ni lazima kutafuta utaratibu tofauti, kamati ya uratibu ilijadili kwa kirefu na kwa kina namna ya kugawa wanafunzi katika mikondo inayoweza kufundishika katika misingi na maadili ya utoaji taaluma na zaidi sana kutofautisha utoaji wa taaluma kwa wanafunzi wanaosoma programu za diploma na wale wanaosoma shahada. Sababu ya pili ni kwamba, masomo ya sayansi yanahitaji uzito wa pekee tofauti na masomo ya sanaa yasiyohusisha vitendo katika maabara. Baada ya mjadala mrefu, ilikubalika kugawanywa mikondo (streams) ya ufundishaji kwa utaratibu ufuatao;

a. Masomo yote ya UALIMU yawe na wanafunzi 120 katika mkondo mmoja.

b. Masomo yote ya SAYANSI ASILIA yawe na wanafunzi 80 kwa mkondo mmoja.

c. Masomo yote ya TEHAMA yawe na wanafunzi 60 kwa mkondo mmoja

2 Kwa mtiririko huo hapo juu, ina maana kwamba kwa kila somo, itabidi wanafunzi wagawanywe katika mikondo kwa idadi iliyokubalika na si kuwarundika wote sehemu moja. Utaratibu huu ndio ulioonekana kutenda haki katika ufundishaji wa vijana hawa kwa kufuata misingi na maadili ya utoaji elimu. Kamati hii ilianza kazi vizuri. Vijana takriban 2000 walipokelewa, wakafundishwa na (semester) huhula wa kwanza ukamalizika vizuri bila migogoro mikubwa.

Pamoja na kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza katika semester/muhula wa kwanza (2014/15)
, ufundishaji ulifanyika kwa ufanisi. Matatizo yalianza kujitokeza pale waalimu walipotakiwa kulipwa kwa kufanya kazi ya ziada katika ufundishaji wa hawa vijana. Kulingana na mapendekezo ya SC ambayo yalikuwa yamekubalika, kila mwalimu aliyefundisha masomo ya DE-SMICT kama somo la ziadi alitakiwa kulipwa Shilingi Milioni Moja (endapo tu somo hilo litakuwa ni ziada katika idadi ya masomo anayoruhusiwa kufundisha). Mvutano wa kuwalipa waalimu hawa ulipelekea wanafunzi kuchelewa kuanza masomo yao ya muhula wa pili kwa wiki mbili. Makamu Mkuu wa Chuo (VC) alipoligundua hili aliamuru malipo yafanyike na baada ya malipo wanafunzi walirejea madarasana na kazi ikaendelea. Mgogoro huu ulipelekea aliyekuwa mwenyekiti wa SC ambaye ni Mkuu wa Koleji ya Elimu kuondolewa katika wadhifa huu. Hatimaye Dean wa Skuli ya Elimu ya Ualimu aliteuli[truncated by WhatsApp]
[5/30, 17:42] br kingu: Kutokana na ufanisi uliopatikana katika mwaka wa masomo 2014/15, Serikali na UDOM waliamua kuleta tena wanafunzi wengine kwa muhula wa 2015/16. Idadi ya hawa wanafunzi ni takriban 6000. Kulingana na idadi hii kuwa kubwa mno, upatikanaji wa waalimu wa sayansi wanaoweza kuenea/kutosha mikondo yote iliyogawanywa ulishindikana.

Hali ya wingi mkubwa wa wanafunzi na upungufu mkubwa wa waalimu ililazimu kubuniwa mbinu za ziada ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaingia madarasani. Kwa maneno marahisi kabisa, kundi hili la pili lililodahiliwa na

3 kusajiliwa ambalo lilikuwa na wanafunzi takriban 6000, lilifanya UDOM

KUELEMEWA na MZIGO. Koleji na Skuli zinazohusika kuwafundisha vijana hawa zilibeba MZIGO uliowazidi kwa kilo/tani nyingi kuliko ilivyopaswa kubeba. Jedwali Namba 1 ni ushahidi wa mzigo unaobebwa na idara mbalimbali;

Kwa ushahidi uliotolewa katika jedwali Namba 1, yeyote hahitaji kutafuta elimu ya ziada kugundua kwamba idara husika zimeelemewa na mizigo ya ufundishaji. Kwa
taarifa tu, mgawanyo wa masomo ya ufundishaji ulioelezwa kwenye jedwali 1 hauhusishi masomo ya Shahada, Diploma za kawaida, Astashahada, cheti na shahada za juu. Hii inadhihirisha wazi kwamba, mzigo kwa walimu wanaofundisha masomo ya sayansi tayari umeshawazidi na bado wanahitajika kufundisha masomo mengine ya kawaida. Kwa vyovyote vile, jitihada zozote za kutafuta suluhu ya mgogoro uliopo zililazimu kuwepo na ushirikiano wa karibu kati ya Menejimenti ya Koleji husika na Utawala Mkuu wa Chuo yaani Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma (DVC-ARC) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala (DVC_PFA). THTU na UDOMASA ilishauri toka mwanzo umuhimu wa ushirikiano wa wadau mbalimbali ndani ya chuo katika kulishughulikia suala la ufundishaji wanafunzi hawa. THTU ilitoa tamko Januari 2015 kuelezea namna isivyoridhishwa na mtindo wa kushughulikia matatizo yanayojitokeza. Tunaweka nukuu mbili tu kati ya mengi ya tamko hilo ambalo lililalamikiwa sana na kufikia hatua ya kutaka kuwajibisha viongozi wa THTU. Hali iliyoelezwa mwaka jana 2015 imejirudia tena mwaka huu 2016 na kuibua mgogoro;

a. Pia kwa nyakati mbalimbali chama cha wafanyakazi (THTU-UDOM) na jumuiya ya wanataaluma (UDOMASA) mara kadhaa walishauri menejimenti ya chuo kushirikisha wafanyakazi wa kada mbalimbali katika hatua zote za maandalizi ya programu hii ili kuleta ufanisi katika kuwaandaa walimu hawa wa masomo ya sayansi.

b. Tunaishauri menejimenti ya chuo na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza kwa wanafunzi wa diploma ya sayansi kwa kuleta vifaa vya maabara, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, usafiri ndani ya chuo, na kuwa na uratibu na usimamizi ulio wazi katika kila idara na kada inayohusika moja kwa moja kuwahudumia wanafunzi hawa. Hii itasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazoibuliwa na wafanyakazi na wanafunzi katika utoaji wa huduma.

2. Kutumia Wafanyakazi wasio wanataaluma

Kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi, kamati ya uratibu ilipendekeza kwenye menejimenti ya UDOM kwamba wafanyakazi ambao si wanataaluma lakini walisoma shahada ya masomo ya sayansi wapewe masomo ya kufundisha kwa makubaliano ya kulipwa baada ya kazi. Wazo hili lilikubalika na kutekelezwa kwa nia ya kutumia rasilimali watu iliyopo ndani ya UDOM badala ya kuwaleta watu wengine kutoka nje ya UDOM. Hata hivyo, waswahili husema,

5 shukurani ya punda ni mateke. Methali hii imejidhihirisha katika hili baada ya watu hawa walioombwa na Menejimenti ya UDOM kusaidia kupunguza upungufu wa walimu wa sayansi kuishia kupewa barua za ONYO ya kwamba walijipa majukumu yasiyowahusu.

3. Jitihaada za uongozi wa Koleji ya Sayansi Kavu na Hisabati (CNMS)

Ili kuhakikisha kuwa wanafunzi hawarudi nyumbani wala kwenda barabararani, uongozi wa CNMS ulijitahidi kuushirikisha uongozi wa chuo na kuomba msaada kila palipoonekana kuhitajika msaada huo. Baadhi ya maswala muhimu yaliyotakiwa kushuhulikiwa ni kuwaongezea uwezo wa kupata waalimu wa ziada, kupata sehemu za kufundishia na kupata vifaa vya maabara. Hata tunapoandika hivi sasa, DVC-PFA, pamoja na kupokea nyaraka mbali mbali zinazomwomba aagize vifaa na madawa ya maabara (laboratory equipments and reagents) hajanunua hata kitu kimoja. Wanafunzi wamefundishwa bila kupewa mazoezi ya vitendo yanayokidhi mahitaji kwa sababu za kiburi cha DVC-PFA. Katika jitihada za kutafuta waalimu wa ziada, DVC-ACR amekataa katakata kutoa mwongozo wa kimaandishi ama ushauri wowote utakaowasaidia viongozi wa CNMS kuboresha hali ya ufundishaji. Aliyekuwa Mkuu wa Koleji ya CNMS anaweza kuonyesha nyaraka ambazo alizituma kwa viongozi hawa wawili wa juu akiomba msaasda bila majibu. Kama kuna watu waliozembea katika kazi hii ni DVC-ARC na DVC-PFA. Kwa mdomo, DVC-ARC alimshauri aliyekuwa Mkuu wa CNMS atumie sera ya uzito wa kazi kutatua suala la uhaba wa waalimu. Hili lisingaliwezekana.

4. Sera ya Uzito wa Kazi (waorkload policy)

UDOM imetengeneza sera ya uzito wa kazi (Workload Policy) ili kusimamia utekelezaji wa utoaji wa taaluma ndani ya chuo. Sera hii ilitokana na; pamoja na mambo mengine, usumbufu mkubwa ulioletwa na walimu wa muda (part time instructors) kutoka vyuo vingine waliokuwa wanapewa mikataba ya kufundisha kuziba pengo la uhaba wa walimu. Sera hii imesaidia sana kupunguza adha iliyokuwa inatokea kabla ya kutengenezwa kwake. Sera hii imeeleza kwa uwazi wa namna ya kugawa uzito wa kazi kwa kila mwanataaluma kama ifatavyo;

6 a. Mkufunzi Msaidizi (Tutorial Assistant - TA) ambaye hana likizo ya masomo lazima afundishe somo moja la diploma na kusimamia semina ya shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe

b. Mkufunzi Msaidizi (Tutorial Assistant - TA) ambaye ana likizo ya masomo lazima afundishe somo moja la diploma au cheti. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe

c. Mhadhiri Msaidizi (Assistant Lecturer – AL) ambaye hana likizo ya masomo lazima afundishe masomo mawili ya shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe

d. Mhadhiri Msaidizi (Assistant Lecturer – AL) ambaye ana likizo ya masomo lazima afundishe somo moja la shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe

e. Mhadhiri (Lecturer), Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecturer) na Profesa ambaye hana majukumu ya madaraka lazima afundishe masomo matatu kuanzia ngazi ya shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe.

f. Mhadhiri (Lecturer), Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecturer) na Profesa ambaye ana majukumu ya madaraka lazima afundishe somo moja kuanzia ngazi ya shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe.

g. Ukubwa wa darasa (class size) itashughulikiwa na kila Koleji lakini

hairuhusiwi kugawa darasa moja zaidi ya mara tatu hata kama lina wanafunzi zaidi ya 3000.

h. Kuhusu mapato yatokanayo na programu zote ambazo si za shahada (Non degree Programs), sera inatamka kwamba 70% ya mapato hayo yapelekwe kwenye Koleji husika ili kuimarisha utoaji wa taaluma. 30% inabaki utawala mkuu kwa ajili ya shughuli muhimu kama utoaji vyeti na mengine.

Tumeamua kutaja sera hii ili kuonesha namna ambavyo isingewezekana kutumika kushughulikia ufundishaji wa wanafunzi wa DE-SMICT ambao wanahitaji uangalizi wa pekee. Hii itasaidia kuondoa upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu ndani ya menejimenti ya UDOM kwamba Diploma husika inaweza kuhudumiwa kwa kutumia sera hii. Limekuwepo jaribio kubwa la Menejimenti kulaz


imisha jambo hilo

7 litokee kwa sababu wanataka kukumbatia mapato yanayotokana na Diploma hiyo huku wakiwadhulumu wanafunzi na waalimu kwa KUKATAA KUANDAA

MAZINGIRA MUAFAKA YA KUFANYA KAZI HII.

DVC-PFA na DVC-ARC wanalazimisha sera hii itumike pale wanapotaka kukwepa jukumu la kununua vifaa vya kufundishia, kukwepa kuwalipa waalimu na kulazimisha ULIPUAJI KAZI. DVC-ARC na DVC-PFA hawataki kabisa kukumbuka sera hii inaafiki kutolewa asilimia 70% ya mapato kwa Koleji husika.

5. Mgogoro Uliosababisha Wanafunzi kutofundishwa

Kutok[truncated by WhatsApp]
[5/30, 17:44] br kingu: Kutokana na maelezo yote hapo juu, jambo moja linajitokeza hapa, Koleji zinazofundisha DE-SMICT zimezidiwa na kazi hasa CNMS na Koleji ya Elimu (CoEd). Kutokana na kuzidiwa huko, hivi majuzi imeibuka mgogoro uliopelekea wanafunzi kutofundishwa. Mgogoro huu unafana na ule wa kipindi cha masomo cha mwaka 2014/15 uliopelekea SC kuundwa upya kama ambavyo nukuu mbili zimewekwa hapo juu. Sisi chama cha wafanyakazi (THTU) tawi la UDOM, tunaamini kwamba mgogoro huu umesababishwa na mambo yafuatayo;

5.1 Utamaduni wa bora liende unaolazimishwa na DVC-PFA pamoja na DVC-ARC

Katika mgogoro huu, DVC ARC na DVC-PFA wamekataa katakata;

1. Kununua vifaa vya maabara kwa ajili ya kufundisha waalimu hawa wa sayansi;

2. Kuusaidia uongozi wa CNMS na CoEd kupata waalimu kwa idadi inayokidhi mahitaji;

3. Kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kuhakikisha kazi inafanyika katika ubora unaowezekana na kukubalika;

4. Kuwalipa waalimu kila inapotakiwa kufanya hivyo; Na;

5. Kusema ukweli kwa Waziri, Katibu Mkuu na Watanzania kuhusu hali halisi ya uendeshaji wa mafunzo haya.

8 Uzembe huu wa DVC-PFA na DVC-ARC pamoja na kiburi cha makusudi ndiyo chanzo cha hali ilivyo hivi sasa ambapo takriban kwa WIKI TATU SASA WANAFUNZI HAWA WA DE_SMICT WANAOCHUKUA MAFUNZO CNMS na CoED HWAJAINGIA MADARASANI.


Imedhihirika pasipo shaka kwamba viongozi hawa wawili bila kujali uharabifu unatokea kwa wanafunzi, chuo na Taifa kwa jumla wanapendelea utendaji kazi na utamaduni wa BORA LIENDE pale wanapotakiwa kuwajibika.

Badala ya kufanya kazi hii kwa ari, weledi na uaminifu kama ilivyostahili, viongozi hawa wawili wameamua kuwa waongo, wasiojali maslahi ya wanafunzi na umma na taasisi wanayoiongoza katika ujumla wake. Badala ya kushirikiana na wahusika kutatua changamoto zinazojitokeza, wameamua kukaa ofisini na kutafuta suluhisho kwa njia ya simu na kuandika barua. Kikubwa kinachokifanywa na DVC-ARC pamoja na DVC-PFA ni kutoa taarifa za uongo kwa viongozi wa Serikali waliojaribu kuingilia hili swala ili kunusuru hali kwa kubambikia watu wasiowapenda makosa na kuanza kushughulika nao badala ya kutatua taizo.

Ni vema tukaweka kumbukumbu sahihi kwamba, Makamu Mkuu wa Chuo Prof

Idriss Kikula tunamtoa katika hili. Tunaamini yeye binafsi angekuwepo, suala hili lisingefika hapa tulipo sasa. Yapo matukio yanayoonesha kwamba tangu mwanzo wa kudahiliwa wanafunzi, DVC-ARC na DVC-PFA hawajawahi kuwa na nia njema ya kuona mambo yanakwenda vizuri. Baadhi ya mambo hayo ni

a. Kumdanganya aliyekuwa waziri wa Elimu Dr. Shukuru Kawambwa kwamba vifaa vya kutosha vipo wakati ni uongo mkubwa. Hili ni bora liende.

b. Kudiriki kulazimisha Diploma hii maalum iingie kwenye mfumo wa kawaida ya utoaji elimu wakati ilishaelezwa toka awali kwamba hii ni programu maalum, hili pia ni bora liende.

c. Kutokuwa tayari hata siku moja kukaa meza moja na walimu wanaofundisha masomo hayo ili kufahamu tatizo la ziada. Badala yake wanamlazimisha Mkuu wa Koleji kutatua mgogoro bila kumpa nyenzo, Bora liende linahusika

9 d. Kukiuka makubaliano halali yaliyofikiwa ya kuunda kamati ya kushughulikia mgogoro huu wakati Naibu Waziri Elimu na Katibu Mkuu walipokuja UDOM. Menejimenti ya UDOM ilikataa majina yaliyopendekezwa na UDOMASA kuingia kwenye kamati na kuwachagua watu wao inaowafahamu kuwakilisha UDOMASA. Hii peke yake inaonesha dhahiri kwamba hawana chembe ya nia kutatua mgogoro isipokuwa bora liende.

e. Kusimamia misingi ya ubabe, vitisho, dharau na kutojali pale inapofuatwa na viongozi wa UDOMASA na THTU kuangalia namna y atika mazingira hayohayo magumu mpaka hali ilipoanza kubadilika.

6.      Mazingira magumu ya ufundishaji wa wanafunzi ambapo waalimu wamekuwa wanayalalamikia kwa muda mrefu sana tangu program hii ilipoanza. Mgogoro huu umepotoshwa kutokana na ukweli kwamba waalimu wanalazimika kufundisha historia ya sanyansi badala ya sayansi kwa vitendo.Ukosefu wa nafasi na vifaa vya maabara ni tatizo kubwa ambalo limelalamikiwa kwa muda mrefu lakini hoja inayoonekana zaidi ni malipo ya waalimu. Mfano katika Chuo cha Sayansi Asilia na Mahesabu kinachohusika na masomo ya Fizikia, Kemia, Baolojia na Hesabu maabara zake hazina vifaa vya kutosha kukidhi mahitaji ya ufundishaji pamoja na koleji husika kutuma maombi karibu kila mwaka.

Mapendekezo ya ufumbuzi

UDOMASA tunaamini kwamba kama  Menejimenti ya chuo ingeonesha ushirikiano wa karibu kwa waalimu wanaofundisha program hii na kushirikiana nao mambo haya yasingetokea au yasingekuwa makubwa kiasi hiki hivyo tunapendekeza yafuatayo kufanywa ili kuweza kutatua mgogoro huu

Kuwepo mawasiliano na ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, Menejimenti ya chuo, Menejimenti za Koleji husika na walimu.Kuangaliwa na kutatuliwa kwa changamoto nyingine zilizoibuliwa na wanataaluma na wanafunzi katika uendeshaji wa program hii badala ya kujikita kwenye suala la malipo tuSerikali kuwa na utaratibu wa kuwasiliana na waalimu na wanafunzi mara kunapotokea matatizo vyuoni ili kupata taarifa toshelezi toka pande zote.

IMETOLEWA NA KAMATI TENDAJI YA UDOMASA

Tarehe 31/5/2016


About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top