Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: JERY MURO AONGOZA MASHABIKI WA YANGA WATOA SHILINGI MILLIONI MOJA KWA MANARA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wanachama na mashabiki wa Yanga, usiku huu wametua nyumbani kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara na k...

Wanachama na mashabiki wa Yanga, usiku huu wametua nyumbani kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa



Simba, Haji Manara na kukabidhi mchango wao kwa ajili ya matibabu.



Wanayanga hao waliongozwa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro na walimkabidhi Manara kiasi ya Sh 1,055,000 kama mchango wao.


Wiki iliyopita, Manara aliamka jicho la kushoto halioni. Pia jicho lake la kushoto halioni vizuri pia. Hivyo anatarajiwa
kupelekwa India kwa ajili ya matibabu na safari yake huenda ikawa Jumamosi hii.



Wanayanga hao walichanga fedha hizo kupitia makundi mbalimbali ya mitandao ya Wanayanga.

“Nashukuru sana wenzangu, mchango huu mnaweza kuuona ni mdogo sana. Lakini ni mkubwa sana kwa kuwa gharama ni kubwa sana.

“Nyie sasa mmredusha zile enzi za Yanga na Simba ambao walikuwa wakiishi undugu wa enzi zile. Msiba wa Yanga  wanazika Simba, Yanga wanazika Simba.
Hivyo ni jambo zuri sana,” alisema.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top