Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: SINEMA YA VYAMA VYA USHIRIKA MKOANI KAGERA YAENDELEA KINGINE HIKI HAPA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Chama   cha   ushirika   cha   Nguvumali   kimeshindwa   kununua   kahawa   msimu   huu   wa 2016/2017 kwa   madai   ya   wanachama    1...

Chama  cha  ushirika  cha  Nguvumali  kimeshindwa  kununua  kahawa  msimu  huu  wa 2016/2017 kwa  madai  ya  wanachama   117  waliopewa  mkopo   kutoka  shirika  la  hifadhi  ya  Jamii  NSSF  Kushindwa  kurejesha  mkopo  huo  kwa  wakati  hivyo  kukosa  fedha  za  kununulia  kahawa.

Akizungumza  na  chombo  hiki  kwa  njia  ya  simu  mwenyekiti  wa  Nguvumali  XAVERY  France  amesema  kuwa  kutokana  na  baadhi  ya  wanachama  kushindwa  kurejesha  mkopo  huo  imekuwa  ni  vigumu kukopa  tena  fedha  kwenye  taasisi  za  fedha   kwa  ajili  ya  kununua  kahawa  kwasababu  bado  wanadaiwa  na  NSSF  amesema  walipatiwa  kiasi  cha  shilingi million 950  na  kuwakopesha  wanachama  lakini  imekuwa  vigumu  kurejesha.


France  amesema  kutokana  na  hali  hiyo wanachama  wa  Nguvumali  kupitia  mkutano  mkuu  walipitisha  azimio  la  kuwapeleka  mahakamani  wanachama  waliokopa  na  kushindwa  kurejesha  fedha  hizo  ambapo  ameeleza  kuwa  baadhi  yao  mahakama  imeishatoa  hukumu  na  julai  23  mwaka  huu dalali  wa  mahakama  yaani  Court  Breka  atawasilisha  kusudio  la  kukamata  mali  za  wanachama  hao  na  kuzipiga  mnada.

Amesema  kutokana  na  hali  hiyo  tayari  shirika  la  hifadhi  ya  Jamii  NSSF  limetoa  muda  wa  kufikia  hadi   tarehe  20  mwezi  wa  nane  kuhakikisha  mkopo  huo  uwe  umerejeshwa.

Hata  hivyo  mwenyekiti  huyo  wa  Nguvumali  amewataka  wanachama  hao  waliochukua  pesa  hiyo  ya  mkopo  wa  NSSF  watambue  kulipa  ni  lazima  wala  siyo  hiari  hivyo  wafanye  kila  liwezekanalo  kuhakikisha  wanalipa  kabla  ya  hatua  kali  za  kisheria

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top