Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: UMMY MWALIMU ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE KIILIMA-BUKOBA AWATAKA WANAKAGERA KUWA NA MOYO WA UZALENDO WA KUWAJALI WAZEE
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametoa wito kwa watanzania hasa Wanakagera kurejere...




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametoa wito kwa watanzania hasa Wanakagera kurejerea moyo wa uzalendo na kupendana kwa kuwatunza Wazee bila kuwatelekeza katika Makazi ya kuwatunza wazee ambao hawajiwezi kwa sasa na wanahitaji msaada wa karibu.



Waziri Ummy aliyasema hayo alipotembelea Makazi ya kuwatunza wazee Kiilima Wilayani Bukoba Mkoani Kagera katika ziara yake  tarehe 16.07.2016 na kujionea changamoto mbalimbali zinazoyakumba makazi hayo ambayo yapo chini ya Wizara yake.



Waziri Ummy, alitoa kauli hiyo kwa jamii hasa kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera kuyatembelea makazi hayo na kuwafariji wazee hao ambao wanahitaji jamii kuwajali mara baada ya kuwahoji baadhi ya wazee wa Makazi ya Kiilima hasa mara baada ya baadhi ya wazee kumweleza kuwa waliletwa na watoto wao wenyewe na kuwatelekeza katika makazi hayo.



Ili kutatua changamoto za makazi hayo ya Kiilima Waziri Ummy alisema kuwa Wizara yake imetenga bajeti ya shilingi bilioni 2.4 kwa ajili ya chakula na  kukarabati Makazi 17 ya wazee nchini lakini alisema tayari amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara kutembelea makazi yote na kuona yale ambayo yana hali mabya ili yahudumiwe kwanza.




“Tutachukua hatua za Haraka sana makazi haya ya Kiilima yana hali mbaya sana na changamoto zake ni kubwa kuliko sehemu nyingine lakini nikifika Wizarani nitamwagiza Katibu Mkuu ahakikishe angalau anaanza kuwajengea vyoo wazee hawa ili kuwanusuru maana hali ni mbaya sana hapa.” Alisema Waziri Ummy.


Aidha, Waziri Ummy aliwaagiza Maafisa Ustawi wa Jamii kuwatembelea wazee hao mara kwa mara ili kuwapatia msaada wa kisaikolojia na kutambua Wazee ambao bado wanao ndugu na jamaa waweze kusaidiwa i kurudishwa kwa ndugu na jamaa zao.



Pia  Waziri Ummy Mwalimu alisema kuwa kwasasa Wizara yake imeamua kubadilisha jina badala ya kuendelaea kuitwa Vituo  vya kuwatunza Wazee sasa yanaitwa Makazi ya wazee, jina la “vituo” ilionekana kuwa ni kama kuwanyanyapaa wazee hao.



Changamoto zinazoyakabili makazi ya wazee Kiilima ni ubovu wa miundombinu kama vyoo, bweni moja ndilo linalotumika la wanawake badala ya mabweni mawili, majengo yote yamechoka yanahitaji urabati pia kuna tatizo la uhaba wa chakula, huduma za afya na usafiri wa kuwasafirsha Wazee kwenda kwenye matibabu, aidha, watumishi wa kituo hicho hawatoshi.





Makazi ya Wazee Kiilima yanawatunza Wazee 18 Wanawake 4 na Wanaume 14. Wazee hao walimshukuru Mhe. Waziri Ummy kwa kuwatembelea na kujionea changamoto walizo nazo katika makazi yao, pia walimshukuru mlezi wao Bi Gladness Rwiza kwa kujitoa kwa hali zote katika kuwahudumia hasa katika upande wa chakula.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top