Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: TASAF TUMAINI JIPYA KWA KAYA MASKINI HAPA TANZANIA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
MPANGO    wa kunusuru kaya maskini    TASAF awamu   ya   tatu   ni   mkombozi   wa wananchi   wanaoishi  kwenye   Kaya   zenye   umasikini  ...
MPANGO    wa kunusuru kaya maskini    TASAF awamu   ya   tatu   ni   mkombozi   wa wananchi   wanaoishi  kwenye   Kaya   zenye   umasikini   uliokithiri  kutokana na baadhi ya waliofanikiwa kupata mradi kutumia pesa hiyo vizuri na kujiinua kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa na  mkurugenzi mtendaji wa TASAF makao makuu Taifa LADISILAUS MWAMANGA  katika kikao cha kuwajengea uelewa  wakuu wa Wilaya wapya kuhusu  utekelezaji  wa kazi za tasaf awamu  ya tatu  wa kunusuru  kaya  zenye  umasiki uliokithiri.

MWAMANGA amesema kuwa   lengo   mahususi  la Tasaf   awamu   ya  kwanza     na   ya pili   kwa jamii ilikuwa kupunguza umasikini  ndio chanzo cha kujenga mashule Vijijini,Zahanati lakini hao masikini waliolengwa wakawa hawezi kupata huduma hizo muhimu.

Amefafanua kuwa    baada ya kujenga mashule,zahanati kwa ajili ya kupunguza umasikini  kwa jamii   bado wakashindwa kupata huduma hizo wakaendelea kubaki na umasikini wao wakaendelea kutokujua kusoma na kuandika.

Amebainisha kuwa   katika majaribio ya Vijiji 40 watoto  waliondikishwa shule walikuwa zaidi ya 1648 ambao walikuwa hawawezi kwenda shule kutokana na umasikini ambapo amefafanua kuwa  kupitia majaribio hayo waliweza kubaini changamoto ya watoto kutoenda shule ni umasikini  na mpango wa tasaf awamu ya tatu,ulipoanza idadi ya watoto walioenda shule iliongezeka.

Baadhi  ya wanufaika walioudhulia kikao hicho ambao ni Editha Muheleza,mkazi wa Kijiji cha Bujugo Bukoba, amesema kuwa  TASAF imemsaidia kupitia mradi wa kunusuru kaya masikini ameweza kuwapeleka  shule   watoto watatu yatima anaoishi nao.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top