Unknown Unknown Author
Title: KAMATI YA MADAWATI KAYANGA YAKABIDHIWA MADAWATI YAKE KUTOKA KWA MZABUNI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kamati ya utengenezaji wa madawati kata ya Kayanga wilayani Karagwe mkoani Kagera imekabidhi jumla ya madwati 250 yenye thamani ya shill...

Kamati ya utengenezaji wa madawati kata ya Kayanga wilayani Karagwe mkoani Kagera imekabidhi jumla ya madwati 250 yenye thamani ya shilling milioni 12 na laki tano kwa uongozi wa kata ya Kayanga baada ya kukamilisha utengenezaji wake.


Akipokea madawati hayo afisa mtendaji wa kata ya Kayanga Nestory Mtungirehi amesema kuwa kwa maagizo ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri  kila kata ilitakiwa kutengeneza madawati 250 na leo kata ya Kayanga ndipo wamekamilisha madawati hayo na watayagawa  kwa shule tano zilizopo ndani ya kata kulingana na mahitaji.

Amesema kuwa shule tano za kata ya Kayanga zote kwa ujumla zilikuwa na mahitaji ya madawati 1511 na yaliyokuwepo ni 1030 hivyo walipungukiwa madawati 481 huku akifafanua jinsi shule hizo zitakavyopokea madawati hayo kulingana na mahitaji yake.


Mtungirehi ameshukuru wananchi wote wa kata ya Kayanga pamoja na wadau wengine waliojitolea kuchangia madawati na kuwataka wale ambao bado walikuwa hawajachangia kuchanga mchango huo mara moja ili waweze kukamilisha pesa ambayo bado wanadaiwa.Naye diwani wa Kata ya Kayanga Adventina kahatano ametoa wito kwa wanafunzi kwa kushirikiana na walimu na kamati za shule  kutunza madawati hayo vizuri ili yaweze kudumu kwa muda mrefu kwa ajili ya kizazi kilichopo na kijacho kwa maendeleo ya Kayanga na Tanzania kwa ujumla.Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya utengenezaji wa madawati kata ya Kayanga Onesmo Rwamasa ameeleza kazi kubwa iliyokuwa inafanywa na kamati hiyo hadi kufanikisha zoezi la utengenezaji wa madawati kwa muda huu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top