Unknown Unknown Author
Title: WANANCHI WA KATA KAMULI WILAYANI KYERWA WAPONGEZWA KWA UCHANGIAJI MADAWATI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi wa kata Kamuli wilayani Kyerwa mkoani Kagera wamepongezwa kwa jitihada   zao ambazo wamezionyesha katika kufanikisha uchangiaji...

Wananchi wa kata Kamuli wilayani Kyerwa mkoani Kagera wamepongezwa kwa jitihada  zao ambazo wamezionyesha katika kufanikisha uchangiaji na utengenezaji wa madawati kwa kufikisha idadi iliyokusudiwa.


Pongezi hizo zimetolewa na diwani wa kata ya Kamuli Jonas Vedasto wakati akiwautubia wananchi kwenye mkutano hadhara katika kijiji cha Rwabigaga katani humo.


Vedasto amesema anawapongeza wananchi pamoja na viongozi wa eneo hilo kutokana na jitihada   zao za kushirikiana  na  kufanikisha zoezi hilo la uchangiaji wa madawati ili wanafunzi wapate mazingira  rafiki yakujifunzia.Hata hivyo amewaasa wananchi kuendelea kushilikiana na viongozi wao pale inapotokea kuchangia jambo lolote katika kuboresha maendeleo ili kata hiyo iweze kusonga mbele.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top