Unknown Unknown Author
Title: VIONGOZI WALIOCHAGULIWA WATAKIWA KUTIMIZA AHADI ZAO WALIZOZITOA KWA WANANCHI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi Mkoani Kagera wamewataka viongozi waliowachagua kutimiza ahadi zao katika kutatua   kero zinazowakabili   ikiwemo migogoro ya A...

Wananchi Mkoani Kagera wamewataka viongozi waliowachagua kutimiza ahadi zao katika kutatua  kero zinazowakabili  ikiwemo migogoro ya Ardhi na upatikanaji wa huduma bora za kijamii.

 Wamebainisha kuwa viongozi wanaonekana katika maeneo ya wananchi wakati wa kuomba Kura lakini baada ya kuingia madarakani hawaonekani matokeo yake ni wananchi kuendelea kusota na changamoto pasipokutatuliwa.


Wananchi hao wamesema kuwa  ni vyema kuanza kuteleza ahadi  muhimu kama ujenzi wa zahanati,Upatikanaji wa maji safi na salama na vizuizi vya barabarani ambavyo hutumika kuwatoza ushuru wakulima wa mazao.

Kwa upande wake Projestus Patrick Mkazi wa kijiji cha Rwigembe Kata ya Ngenge wilayni Muleba  amesema tatizo la ubovu wa miundombinu ya barabara inaweza kusababisha vifo kwa akina mama wajawazito ambapo viongozi hao wamekuwa wakikwepa kupita katika barabara hizo hali ambayo wananchi wanahisi wahawajui uchungu waoupata wanapotumia miundombinu hiyo

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top