Unknown Unknown Author
Title: WATOTO WAPOTEZA MAISHA KWA KUUNGUA NDANI YA NYUMBA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Watoto   watatu   wa    familia   katika   kijiji   cha   Rwabigaga   kata   Kamuli   wilayani   Kyerwa   mkoani   Kagera   wameungua   ...

Watoto  watatu  wa   familia  katika  kijiji  cha  Rwabigaga  kata  Kamuli  wilayani  Kyerwa  mkoani  Kagera  wameungua  kwa  moto  ndani  ya  nyumba  na  kupoteza  maisha  na  watu  wawili  wanashikiliwa  na  jeshi  la  polisi  kuhusiana  na  tukio hilo.

Tukio  hilo  lililotokea siku  ya  jumatatu ya  julai 04  mwaka  huu  majira ya  saa  kumi  na  moja jioni ambapo  wazazi  wa  watoto  hao  hawakuwepo   nyumbani  na  walikuwa  stesheni  matembezi  ndipo  ajali  hiyo  ya  moto  ilitokea.

Mtendaji  wa  kijiji  cha  Rwabigaga Dafroza Gozbert amewataja  watoto  waliopoteza  maisha  kwenye  tukio  hilo  la  nyumba  kuungua  moto  kuwa  ni  Avith Edson mwenye  umri wa miaka 5 na miezi 2, Eliada Edson  miaka 3 na miezi 3 na  Elieth Alistides miaka 3 na mwezi mmoja ambao wote waliungua katika nyumba moja huku wazazi wao wakiwa hawamo ndani.

Amesema alipofika kwenye eneo la tukio wazazi wa watoto hao walimweleza  kuwa  wakati  tukio  hilo  linatokea  hawakuwepo  na walipata  taarifa  kutoka  kwa  wasamaria  wema  ambao  ni  majirani  zao.

.
Gozbert  amesema  kuwa  baada  ya  taratibu  za kimatibabu  zilizosimamiwa  na  jeshi  la  polisi  miili  hiyo  imeruhusiwa  kuzikwa  na  wazazi  wao  huku  jeshi  la  polisi  likiwashikilia  watu  watatu  kwa  ajili  ya  mahojiano  zaidi  kuhusiana  na  tukio  hilo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top