Unknown Unknown Author
Title: WATAKIWA KUTOTUMIA AU KUUZA POMBE WAKATI WA SAA ZA KAZI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wamiliki   wa   baa   na   vilabu   vya   pombe   wilayani   Karagwe   wametakiwa   kutotumia      au   kuuza   pombe   kwa   saa   za  ...

Wamiliki  wa  baa  na  vilabu  vya  pombe  wilayani  Karagwe  wametakiwa  kutotumia    au  kuuza  pombe  kwa  saa  za  kazi  hadi  majira  ya  saa  kumi  jioni  ili  kutii  sheria  inavyoelekeza  na  atakayeenda  kinyume  na  utaratibu  huo  atachukuliwa  hatua  za  kisheria  kwa  kuikosea  jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania.

Kauli  hiyo  ilibuka  katika mkutano  wa  kutoa  elimu  kwa  walengwa  wa  mpango  wa   TASAF  111 uliofanyika  hivi  karibuni  kwenye  ofisi  ya  kijiji  cha  Kanoni  kata  ya  Kanoni  wilayani  Karagwe  mkoani  Kagera Mwenyekiti  wa  kamati  ya  Elimu,Afya na  maji  Charles  Bechumila  akihamasisha  walengwa  kujiunga  na  mfuko  wa  afya  ya  jamii  yaani  CHF amesema  amechukizwa  na  kitendo  cha  baadhi  ya  wananchi  wa  stesheni  ya  Rwambaizi  kuonekana  wakichoma  nyama  na  kunywa  pombe  saa  za  asubuhi  ambazo  ni  za  kazi.


Amesema  huwezi  kuondokana  na  umaskini  bila  kuwa  na  matumizi  sahihi  juu  ya  kupata  na  kutumia  pia  ameongeza  kuwa  lazima  kuwa  na  afya  ndipo  utapata  nguvu  za  uzalishaji  hivyo  akawataka  walengwa  hao  kujiunga  na  mfuko  wa  CHF kwa  kuchangia  shilingi 15000 kwa  mwaka na  watatibiwa  bure  watu  sita kwa  mwaka  huo  wote.

Kutokana  na  kauli  hiyo  ya  unywaji  pombe  saa  za  asubuhi  mwenyekiti  wa  halmashauri  ya  wilaya  ya  Karagwe  Wallesi  Mashanda  akatoa  kauli  kwa  watendaji  na  kuwataka  kujisimamia  na  kutekeleza  sheria  kukomesha  tabia  hiyo.

Hata  hivyo  amesema  siku  nyingine  akiwa  kwenye  ziara  ya kukagua  shughuli  za  maendeleo  akikutana  na  hali  hiyo  ya  unywaji  wa  pombe  saa  za  kazi  hataivumilia.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top