Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: UPATIKANAJI WA MAJI BADO NI TATIZO SUGU KWA WANANCHI VIONGOZI WAOMBWA KULITATUA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi wilayani Karagwe mkoani Kagera wamewaomba viongozi wao waliowachangua kuangalia kwa karibu suala la upatikanaji wa maji safi na...

Wananchi wilayani Karagwe mkoani Kagera wamewaomba viongozi wao waliowachangua kuangalia kwa karibu suala la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yao kwani ni moja wapo ya ahadi walizohaidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa  mwaka 2015.


Wakiongea na kituo hiki baadhi ya wananchi wa wilaya ya Karagwe wamesema kuwa katika maeneo yao kuna tatizo kubwa la kufuata maji kwa umbali mrefu na maji hayo siyo safi na salama kwa matumizi ya kila siku ya binadamu.

Wamesema kuwa wakati viongozi wao wanagombea nafasi za uongozi walihaidi kuwapatia maji ,hivyo kuwaomba kutekeleza ahadi hiyo kwani ukosefu wa maji unawasababishia wananchi kutoshiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo kwani wakati mwingine wanafuata maji siku nzima .

Diwani wa kata ya Nyakahanga Charles Bechumira ambaye amekiri kuwepo kwa  tatizo la maji katika kata ya Nyakahanga huku akiwataka wananchi kuwa wavumilivu wakati suala hili likifanyiwa kazi na viongozi wa ngazi husika.


Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Karagwe Innosent Bashungwa ameeleza kuwa  anaendelea kufanya jitihada za makusudi ili kutumiza ahadi yake aliyohaidi wananchi wa wilaya ya Karagwe kuhusu kuwasogezea maji karibu huku akieeleza juu ya kuanza kwa mradi mkubwa wa maji utakaosambaza maji wilaya ya Karagwe kutoka katika ziwa Rwakajunju.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top