Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MAENEO YA HIFADHI YATAKIWA KULINDWA KWA FAIDA ZA BAADAE
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodr...

Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues amewakumbusha wadau wa urithi wa dunia na maeneo ya hifadhi kufanyakazi kwa pamoja kwa lengo la kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo bila kuondoa ushiriki wa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.

Kauli hiyo ameitoa katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika hilo  kwa wadau wa mazingira ya hifadhi na urithi wa dunia mjini Marangu Moshi, yaliyofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Resort kufuatia makubaliano na serikali ya Tanzania.



Akizungumza na washiriki amesema kuwa UNESCO inachofanya ni kuanzisha safari ambayo inaweza kuwa ngumu na ndefu lakini washiriki wake ni lazima kutambua namna ya kuendelea kufanya menejimenti ya maeneo ya hifadhi na urithi wa dunia kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho

Akifungua mafunzo hayo ambayo wataalamu ni washiriki wenyewe wakitumia njia ya kuelewa ya methodolojia ya uchambuzi wa vikwazo (Bottleneck Analysis Methodology) amesema safari ya kufanikisha menejimenti ya maeneo hayo duniani na hasa hapa nchini  Tanzania ni yenye changamoto nyingi na kwamba wadau wote wanatakiwa kuwa pamoja kuvishinda vikwazo hivyo na kuifanikisha safari yao.

Rodrigues akizungumza katika  Warsha hiyo ambayo imechukua wadau mbalimbali wa masuala ya urithi na menejimenti zake kutoka serikalini, taasisi zisizo za kiserikali na wananchi wengine, amesema kwamba maeneo hayo yamezungukwa na wananchi na pamoja na kuwawekea sheria za kutoharibu na kuyachakaza ipo haja ya kushirikiana nao namna ya kupanga kuyaendeleza maeneo hayo huku yakiwa yamebaki katika hali inayotakiwa.




Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kupanga maendeleo katika maeneo ambayo ni ya urithi wa dunia, binadamu na maeneo ambayo uhai unaweza kuwepo.

Aidha akifafanua zaidi amesema mafunzo hayo yamelenga kuwapa wahusika nadharia zinazofaa katika safari ndefu ambayo UNESCO nayo itashiriki na isingelipenda kumwacha hata mtu mmoja nyuma.

Mafunzo hayo yanatolewa kufuatia mpango wa UNESCO wa kutaka kuwa na uhakika na kuhami maeneo hayo ya urithi; huku mamlaka zikitoa ushirikiano ili kuwezesha malengo ya maendeleo endelevu, ambayo ndiyo ajenda ya dunia kuelekea 2030, yanafikiwa bila kuathiri maeneo tajwa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top