Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WANANCHI WATAKIWA KUTIMIZA AGIZO LA SERIKALI KUWA NA VYOO BORA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
W ananchi   wa   kata ya Mabira wilayani Kyerwa mkoani Kagera wametakiwa kuzingatia agizo la serikali la kutengeneza vyoo bora ili kuepu...

Wananchi  wa  kata ya Mabira wilayani Kyerwa mkoani Kagera wametakiwa kuzingatia agizo la serikali la kutengeneza vyoo bora ili kuepuka mlipuko wa magonjwa yanayotokana na uchafu.


Wito huo umetolewa na afisa afya wa kata ya Mabira Jackiline Shukuru Gamale wakati akiongea na watendaji wa vijiji,wenyeviti wa vijiji na wahudumu wa afya wa vijiji kuhusu taarifa ya ujenzi wa vyoo bora katika kata hiyo.


Amesema kuwa kila familia inatakiwa kujenga choo bora kwa kutumia saluji hivyo ni jukumu la viongozi kuhakikisha wanahamasisha wananchi wote kuwa na vyoo vya namna hiyo kabla ya muda uliopangwa kufika.

Amesema kuwa ujenzi wa choo bora ni afya ya kila mmoja hivyo nguvu ya serikali itatumika kwa wale ambao watakaidi kufuata agizo hilo.

Gamale amezungumzia pia suala la usafi kwa ujumla akisisitiza kuwa ni la kila siku na sio kusubiri siku ya alhamisi au jumamosi ya kila mwisho wa mwezi

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top