Unknown Unknown Author
Title: WAKULIMA WADAI SIKUKUU YA NANE NANE IFANYIKE KWENYE MAENEO YAO NA SIYO MJINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ili maonesho ya siku kuu   ya wakulima maarufu Nane Nane  yaweze kufanyika ngazi ya Wilaya  inategemea uwezo na Bajeti ya Halmashauri hu...

Ili maonesho ya siku kuu   ya wakulima maarufu Nane Nane  yaweze kufanyika ngazi ya Wilaya  inategemea uwezo na Bajeti ya Halmashauri husika.


Hayo yamebainishwa  na Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Cleophace Kanjagaile wakati akijibu hoja za wananchi kupitia vyombo vya habari waliomba maonesho hayo yaweze kufanyika katika ngazi ya Wilaya ili kuwawezesha  wakulima kushiriki kwa wingi na kupunguza gharama za wao kushiriki maonesho hayo  ngazi ya mkoa.


Amesema miaka 4 imepita bila maonesho hayo kufanyika ambayo  yalikuwa yakifanyika kwa ngazi ya  wilaya katika kata mbalimbali za wilaya hii  na kwamba hayafanyiki kutokana na  kuwa kila halimashauri  ni lazima kushiriki maonesho ya Kikanda ambayo hufanyika Mwanza kanda ya ziwa na  mkoa katika  Manispaa ya Bukoba Viwanja vya Kyakailabwa na ikifanyika  kwa  ngazi  ya  wilaya  zinahitajika  shilingi  million 100 ili  kufanikisha  maonesho hayo.
…………………………Insert………………


Amesema kama  Idara ya kilimo wana wanatambua umuhimu  kusogeza maonesho haya Karibu na wa wakulima  kwani ndio walengwa wakuu lakini wanalemewa kufuatia kuwa maonesho ya Kikanda na mkoa ni ya lazima.

Ametoa wito kwa wadau wa kilimo na maendeleo, Taasisi zakifedha na makampuni mengine  kushiriki kwa pamoja na kuwezesha kufanikisha maonesho hayo endapo watafuatwa pale yatakapofanyika  kwa ngazi ya  wilaya ili kuwawezesha wakulima wasio na uwezo wa kuchangia kushiriki kikamilifu siku yao.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top