Unknown Unknown Author
Title: WAZIRI LUKUVI ATATUA KERO ZA WANANCHI WA KAGERA KUHUSU ARDHI AWAPANGUSA MACHOZI WALIODHURUMIWA ARDHI ZAO MUDA MREFU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi awapangusa machozi wananchi wa Mkoa wa Kagera waliokuwa wamedh...
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi awapangusa machozi wananchi wa Mkoa wa Kagera waliokuwa wamedhurumiwa ardhi zao na walio kuwa  na kero za ardhi za siku nyingi ambapo alisikiliza kero hizo kwa umakini na kuzipatia ufumbuzi wa papo kwa hapo na kutoa haki kwa waliostahili.
Akiwa Mkoani Kagera katika ziara yake ya siku mbili Mhe. Lukuvi aliitumia siku yake ya kwanza ya tarehe 19/8/2016 kusikiliza, kupokea na kutatua kero mbalimbali za muda mrefu na zilizoshindikana  kwa wananchi  kuhusu ardhi ambapo kero nyingi alizisuluhisha na kuzipatia ufumbuzi.Aidha kwa wananchi waliokuwawamejipatia ardhi kwa njia ya udanganyifu au kwa kuwatapeli wananchi wenzao waliamuliwa kurejesha ardhi hizo kwa wamiliki halali wenye hati zinazoonyesha mmiliki halali ni nani pia Halmashauri ya Manispaa iliamuliwa kuwapatia viwanja wananchi ambao walichukuliwa viwanja vyao na kuhaidiwa kupatiwa viwanja vingine ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa Agosti 2016.
Katika kutoa haki kwa wananchi Mhe. Waziri Lukuvi alifuta umiliki wa ardhi ya Bw. George Rogers ambye alikuwa Mtanzania lakini aliamua kuchukua uraia  wa nchi ya Uingereza ambaye alikuwa na mgogoro na wananchi wa kata ya Nyanga katika Manispaa ya Bukoba.


Bw. Rogers raia wa Uingereza alifutiwa umiliki wa ardhi aliyokuwa anaimiliki katika eneo la Kata ya Nyanga Manispaa ya Bukoba kitalu namba 1(b) kilicho kuwa na ekari zaidi ya 1800, pia alifutiwa umiliki wa eneo la Kibuye katika Manispaa ya Bukoba lenye vitalu 9 na kufutiwa pia umiliki wa ekari 60 alizokuwa anazimiliki katika eneo la Bugolora Wilayani Missenyi.Akitangaza kufuta umiliki wa maeneo yote hayo Mhe. Lukuvi Alisema kuwa Bw. Rogers na Kampuni yake ya Rockshild Quality Food Products Ltd hawakufuata utaratibu wa umilikaji wa ardhi bali yeye na Kampuni yake walijipatia ardhi hiyo kwa njia za udanganyifu kutoka kwa wananchi.Aidha Mhe. Lukuvi alisema kuwa raia wa nchi za Kigeni hawaruhusiwi kuingia mitaani na kuanza kujinunulia ardhi kwa wananchi bali wanatakiwa kupitia katika kituo cha uwekezaji (Tanzania Ivestment Center) ambao wanayo dhamana ya kuwapatia wawekezaji au raia wa nchi za nje sehemu au ardhi za kuwekeza mahala popote nchini.


Mbali na kutatua migogoro ya mwananchi mmoja mmoja Mhe. Lukuvi alisema kuwa migogoro mikubwa kama ya wafugaji  na wakulima, mgogoro wa wananchi wa Kakunyu Wilayani Missenyi na Ranchi za Taifa tayari unashughulikiwa na Wizara nne ambazo ni Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, TAMISEMI, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.


Katika hatua nyingine Mhe. Lukuvi alisema kuwa ameamua kugawa majukumu ya wizara yake katika kanda ambapo masuala yote yanayohusu ardhi hayaendi tena Dar es Saalam bali yanamaliziwa katika kanda hizo na Mkoa wa Kagera upo katika Kanda ya Ziwa ambayo ipo jijini Mwanza.Mhe. Lukuvi kwenye ziara yake Mkoani Kagera alifuatana na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Bw. Joseph Shewiyo, Msajili Msaidizi wa Hati Kanda ya Ziwa Bi Magrgeareth Mziray, na Msajili Msaidizi wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Kanda ya Ziwa Bi Dorothy Philip ambapo Wataalam hao wakishirikiana na Maafisa Ardhi wa Halmashauri za Wilaya walimsaidia Mhe. Waziri Lukuvi kupata ufafanuzi wa kero mbalimbali na kupata ufumbuzi wa keo hizo katika Mkutano na wananchi uliofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Bukoba.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top