Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: HATUA ZINAZOENDELEA KUCHUKULIWA NA SERIKALI JUU YA TETEMEKO MKOANI KAGERA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Serikali ya Mkoa wa Kagera leo Septemba 14, 2016 tayari imepokea misaada mbalimabli ya fedha taslimu na mahitaji mbalimbali kama...




Serikali ya Mkoa wa Kagera leo Septemba 14, 2016 tayari imepokea misaada mbalimabli ya fedha taslimu na mahitaji mbalimbali kama Sukari, Mchele, Unga, Maji ya kunywa, Sabuni, Blanketi, Shuka Maharage, matrubali, Mbao na Sementi  vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 32.



Aidha, Kamati ya Maafa ya Mkoa tayari imeanza kugawa mahitaji hayo kwa wananchi waliopatwa na janga la tetemeko na kwa sasa hawana mahala pa kuishi. Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Kashabo Manispaa ya Bukoba wamegawiwa mahita ji hayo na aliyeongo zoezi hilo ni Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe, Meja Jenerali Mstaafu Salim M. Kijuu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya mkoa.




Katika hatua nyingine Kamati ya Maafa ua Mkoa imeamua kutoa bati 20 na sementi mifuko 5 kwa kila mwananchi ambaye nyumba yake ilianguka kabisa au haifai kuishi tena.  Aidha, wapangaji waliokuwa wanapanga katika nyumba hizo watalipiwa kodi ya miezi na Serikali sita kila mwezi 20,000/=





Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu ameandaa kikao cha harambee ya kuchangia maafa mkoani Kagera tarehe 16.09.2016 siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  kuanzia saa 3:00 Asubuhi na anawaalika wadau wote kuja kuchangia katika harambee hiyo.






Aidha kwa wale wanaotaka kuchangia lakini hawatahudhuria wanaweza kuchangia kupitia Akaunti ya Benki iliyopo CRDB inayojulikana kama “KAMATI YA MAAFA KAGERA CRDB BUKOBA” Akaunti Namba. 0152225617300. Tunawashukuru wote wanaoendelea kuchangia na Mungu awazidishie.
Imetolewa na:      Sylvester M. Raphael
              Afisa Habari (Mkoa )
              KAGERA
             
Septemba 14,2016

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top