Unknown Unknown Author
Title: WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA AONGOZA MAMIA YA WANACHI WA KAGERA WALIOKUMBWA NA TETEMEKO LA ARDHI KUAGA MIILI YA MAREHEMU 16
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na: Sylvester Raphael Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa a...
Na: Sylvester Raphael
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya wananchi wa Mkoa wa Kagera waliofurika uwanjani Kaitaba kuiaga miili ya wapendwa wao waliofariki wakati mkoa huo ulipopatwa na janga la tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, 2016 saa 9:00 alasiri na kusababisha vifo vya wananchi 16, kujeruhi  253 pia na kusababisha nyumba 840 kuanguka na nyumba 1,264 kupata nyufa.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwapa pole wananchi wa Mkoa wa Kagera kwaniaba ya Serikali na kusema kuwa Serikali inafanya juhudi zote za kutuma wataalam kuja Mkoani Kagera kuangalia kama tetemeko la ardhi litarudia tena au dalili za lini linaweza kutokea tena ili kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kujikinga na tetemeko hilo pindi linapotokea tena. Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa alisema tayari ofisi yake imetuma Wataalamu wa kitengo cha maafa ili kufika Mkoani Kagera kufanya tathimini ya kina na ya haraka wakishirikiana na kamati ya maafa ya mkoa ili kubaini ni sehemu gani zinazohitaji huduma au msaada wa haraka ambapo janga la tetemeko limesababisha madhara makubwa.Mkuu wa Mkoa  wa Kagera Mhe. Kijuu akitoa taarifa jinsi tetemeko hilo lilivyotokea na madhara yaliyosababishwa na tetemeko hilo alimweleza Waziri Mkuu Kassim majaliwa kuwa tetemeko hilo lilitokea majira ya saa 9:00 alasiri, aidha, tetemeko hilo lilikadiriwa kuwa na ukubwa 5.7 katika vipimo vya Richter na lilisababisha madhara makubwa katika mkoa  mzima.Mhe. Kijuu alimweleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa tetemeko hilo lilisababisha vifo vya wananchi 16, majeruhi waliolazwa katika Hospitali mbalimbali zilizoko kwenye mkoa wa Kagera ni 170, Majeruhi waliotibiwa na kuruhiusiwa ni 83 na jumla ya majeruhi wote ni 253.  Aidha nyumba za makazi zilizoanguka ni 840, nyumba zilizopata nyufa ni 1,264 na  majengo ya taasisi yaliyoripotiwa kuanguka ama kupata nyufa ni 44.

Aidha, Mkuu wa Mkoa alimweleza Mhe, Majaliwa kuwa mara baada ya tetemeko hilo kutokea uongozi wa mkoa ulichukua hatua za haraka kwa kuokoa wananchi na kuwapeleka hospitali mbalimbali kwa ajili ya matibabu. Pili, baadhi ya wananchi wenye nyumaba zilizoathirika walipatiwa makazi ya muda na kuwahamasisha kusaidiana wao kwa wao  kupeana hifadhi. Mwisho Mkoa unaendelea na tathimini ya athari na hasara zilizosababishwa na tetemeko hilo.
Agizo la Waziri Mkuu, Mkoa chini ya Mwenyekiti wa kamati ya Maafa ya mkoa ambaye ni Mkuu wa Mkoa pia na Maafisa kutoka kitengo cha Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu  waendelee kufanya tathmini ya kina ya kubaini athari na hasara za tetemeko hasa kwa kuanza na sehemu zinazohitaji huduma ya haraka kama shule mbili za Sekondari za Ihungo na Nyakato ili Serikali iweze kusaidia mara baada ya kupata tathimini ya hali halisi ya maafa.


Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasiili Mkoani Kagera majira ya saa 7:00 mchana aliwatembelea majeruhi waliojeruhiwa wakati wa tetemeko hilo ambao bado wamelazwa katika Haspitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera, pia alitembelea shule za Sekondari za Nyakato na Ihungo ambako madhara yalitokea makubwa na kupelekea wanafunzi kukosa sehemu za kulala baada ya mabweni yao kubomolewa na tetemeko.

Vile vile Mhe Majaliwa  alishuhudia maiti 14 na kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu katika uwanja wa Kaitaba ambapo marehemu hao  waliombewa dua na sala kutoka kwa viongozi wa dini Mkoani Kagera . Pia Mhe. Majaliwa aliwapa pole wafiwa na kuzungumza na wananchi waliokusanyika uwanjani hapo kwa kuwapa salaam za Serikali.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top