Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WANANCHI WATAHADHARISHWA KUTOPOTOSHWA JUU YA JANGA LA TETEMEKO
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi mkoani KAGERA wametakiwa kuacha kupotoshwa na watu kuhusu kutokea kwa tetemeko la ardhi ambalo limetokea tarehe 10/9/2016 na ku...

Wananchi mkoani KAGERA wametakiwa kuacha kupotoshwa na watu kuhusu kutokea kwa tetemeko la ardhi ambalo limetokea tarehe 10/9/2016 na kusababisha madhara mbalimbali.

Akizungumza na vyombo vya habari katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini PROFESSA JUSTIN NTALIKWA amesema kuwa wapo baadhi ya watu wanaoamini kuwa tetemeko limesababishwa na imani za kishirikiana  ambapo amebainisha kuwa tetemeko halihusiani na shughuli zozote za kibinadamu.

Amebainisha kuwa tukio la tetemeko la aridhi limeanzia kata ya Minziro ambapo amesema kuwa ni kilometa 10 kutoka ardhini amesema kuwa kutokea kwa tetemeko la ardhi mkoani KAGERA kunatokana na kuwa karibu na bonde la ufa.



Akizungumzia jinsi ya kujikinga na tetemeko linapotokea NTALIKWA amesema kuwa wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari na kuepuka kukimbia ambapo amesema tetemeko linatembea umbali wa kilometa 8 kwa sekunde moja huku akibainisha kuwa madhara makubwa yalitokana na watu wengi kukimbia ili kujiokoa.


Kwa upande wake mtendaji mkuu wa wakala wa Jiorojia PRF ABUDULKARIMU MRUMA amesema kuwa tetemeko la ardhi linatokea kwa sababu za kijiorojia na hazisababishwi na kazi nyingine za kibinadamu.


.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wananzia vyombo vya moto pale tetemeko linapotokea ili kupunguza adhari.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top