Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MADREVA WAANZA KUIELEWA KAMPEIN YA ZUIA AJALI HAPA MKOAN KAGERA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
  Baadhi   ya   madreva   katika   mamlaka   ya   mji   mdogo   wa   Kayanga wilayani   Karagwe   wameelezea   umuhimu   wa   Kampeini...
 
Baadhi  ya  madreva  katika  mamlaka  ya  mji  mdogo  wa  Kayanga wilayani  Karagwe  wameelezea  umuhimu  wa  Kampeini  ya  ZUIA  AJALI  HAPA  kuwa  inasaidia  kutoa tahadhari  kwa  watumiaji wote wa  barabara.


 Claudian Andrew ambaye ni dreva tax amesema kuwa ubovu wa vyombo vya usafiri ndio unaosababisha ajali na kuwataka madreva kuwa makini na vyombo vyao na kuepuka kuendesha magari wakiwa wamelewa ili kupunguza ajali zisizotarajiwa

 
Fadhili Sued ambaye ni dreva wa gari la abiria (hiace) amesema kuwa wamenufaika na wameelimika  kupitia kauli hiyo.



 
Sued amewashauri madreva wenzake  wa magari ya abiria kufuata kanuni na sheria za barabara na kuepuka mwendo kasi ili kulinda uhai wa abiria.



 


 Eliza Emmanuel ambaye ni abiria amesema kauli hiyo ya HATUTAKI AJALI TUNATAKA kuishi imesaidia kupunguza ajali kwani madreva wamepunguza mwendo kasi wawapo safarini na amewataka madreva kuendesha magari kwa mwendo ulioruhusiwa na kufuata kanuni na sheria za barabara.

 
Ameishukuru serikali kwa kufuatilia kwa makini  sheria kwa  wanaokiuka masharti ya barabarani. Pia amewataka madreva kupunguza mwendokasi ili kuokoa maisha ya watu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top