Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: UVAMIZI WA VYANZO VYA MAJI BADO NI TATIZO KARAGWE
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi wameaswa   kuacha tabia ya kujimilikisha Ardhi kinyume cha sheria na kutoendesha ghughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya ma...

Wananchi wameaswa  kuacha tabia ya kujimilikisha Ardhi kinyume cha sheria na kutoendesha ghughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji na wanaofanya hivyo kutakiwa kuhama mara moja  kabla sheria hazijachukuliwa.


Agizo hilo limetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mh Walles Mashanda aliptembelea  Kijiji cha Katanda Kata ya Kihanga  Hapa Wilayani Karagwe ili kumaliza migogoro ya Ardhi baina ya wananchi na serikali za vijiji zikiwemo sehemu zenye vyanzo vya maji.


Aidha amemwagiza mwenyekiti wa kijiji cha Katanda kufikia tarehe 31 mwezi huu kuwa ameisha suluhisha migogoro yote katika vyanzo vya maji pasipokufanya hivyo atachukuliwa hatua.



Kuhusu waliovamia Ardhi Mashanda ameuagiza uongozi wa Serikali ya Kijiji kuwa ndio wenye mamlaka na Ardhi hivyo wachukue hatua na taarifa zifike katika ngazi za juu ili sheria zichukue mkondo wake

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top