Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: *BADILIKA, THIS IS 2017*
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Kipenga kimeshapulizwa wenye mbio zao wameshatoka, wewe bado uko kitandani unaandika happy new year kwenye mitandao ya kijamii ...



Kipenga kimeshapulizwa wenye mbio zao wameshatoka, wewe bado uko kitandani unaandika happy new year kwenye mitandao ya kijamii

Kipenga kimeshapulizwa wewe maliza bajet yote leo kwenye starehe alafu uanze kulalamika eti Mwezi wa kwanza Mgumu utadhani umeubonyeza

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaenda na kasi ya Magufuli, wewe bado unapiga vibomu alafu unalalamika uchumi mbovu

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaenda porini kutafuta pesa na kuja kuzitumia mjini wanaenzi ule msemo wa Mali utaipata shambani /porini wewe unatafuta pesa kati kati ya mji, my friend utapata nauli tu

Kipenga kimeshapulizwa wanasiasa wenzako wanaleta matokeo chanya kwenye jamii, wewe umekwama na siasa zako za Maigizo, utaisoma namba vizuri

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatengeneza ajira na kulipa mishahara, wewe umeajiriwa mwaka wa 10 unasubiri bonus, increment na kubagain ongezeko la mshahara alafu bado unataka kuwa celebrity, my friend labda celebrity wa mikopo

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatafuta matatizo ili yawe fursa kwao, wewe ukiona changamoto unakimbia na kuilalamikia serikali, utasubiri sana

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatafuta kazi kwa kufanya kazi za kujitolea kujenga nchi, wewe unasubiri interview, hiyo experience utaipata ndotoni

Kipenga kimeshapulizwa wakati wenzako wanahojiwa na forbes magazine wamewezaje kuleta impact Africa nzima, we unakazana kujisifu unafollowers wengi instagram alafu Huna hata mmoja ambae ni rafiki wa kusaidiana.

Kipenga kimeshapulizwa wakati wenzako wakipost kwenye mitandao yao ya kijamii wanalipwa, wewe kazi yako ni kuretweet/kurepost na kulike siku nzima bila kupata faida yoyote

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaoipenda nchi yao wanachangia matembezi ya tembo na faru yatakayofanyika Morogoro kwa kununua tshirt, wewe bado unazungusha bia na nyama choma alafu unalalamika watalii wamepungua, unataka waje wakuangalie wewe?

BADILIKA This is 2017 my friend.

Juhudi Felix 2017.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top