Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: VIONGOZI WATAKIWA KUTOWAFUMBIA MACHO WATAKAOSHINDWA KUPELEKA WATOTO SHULE
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Viongozi   katika kata   ya   Kabirizi wilayani Muleba mkoani Kagera wametakiwa kutowavumilia wazazi wanaoshindwa kuwapeleka watoto wao ...

Viongozi  katika kata  ya  Kabirizi wilayani Muleba mkoani Kagera wametakiwa kutowavumilia wazazi wanaoshindwa kuwapeleka watoto wao shule.

Katibu tawala wa wilaya ya Muleba  Benjamini  Mwikasyege  amesema hayo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Muleba  wakati wa mkutano wa wananchi wa kijiji hicho .

 Mwikasyege  amesema kuwa serikali  inaitaji wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza wanakwenda shule hivyo atakayeshindwa kumpeleka mtoto shule kwa makusudi serikali  haitomvumilia na itapata nafasi ya kumsukuma kupeleka mtoto shule

Amesema kuwa viongozi wote kuanzia ngazi ya kijiji katika wilaya ya Muleba wameshapokea maelekezo kutoka kwa mkuu wa wilaya kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanakwenda shule kwa muda muhafaka.


Wakati akisoma taarifa ya kata hiyo  kaimu afisa mtendaji wa  kata   Nicodemus Mkata  amesema kuwa  kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na upungufu wa walimu 44 pamoja na baadhi ya bara bara kupitika kwa shida.


Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika kata hiyo ni 128 ikiwa wavulana ni 64 na wasichana 64.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top