Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: TAASISI ISIYO YA KIRAIA YATOA SARUJI MIFUKO 100 KUSAIDIA WANANCHI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Taasisi isiyokuwa ya    kiserikali ya Mhola imetoa mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule...

Taasisi isiyokuwa ya   kiserikali ya Mhola imetoa mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Kashanda iliyoko katika kata ya Kabirizi wilayani Muleba.

Mkurugenzi wa Taasisi  ya  Mhola  Saulo Malauri  inayotoa msaada wa kisheria pamoja na kushugulika na maendeleo ya jamii hasa katika kitengo cha malezi na makuzi ya watoto wameguswa  sana na upungufu wa madarasa katika shule hiyo.

 Malauri amesema kuwa mtoto anaposomea katika mazingira magumu inaweza kumpunguzia uwezo wa mtoto kupenda shule hivyo wataendelea kushirikiana na viongozi wa kata hiyo kuhakikisha wanapunguza changamoto zinazowakabili.


Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Salmoni Karugaba amesema kuwa shule hiyo ina upungufu wa vyumba 15 vya madarasa ambapo vyumba vinavyotakiwa kwa shule nzima ni 23 na vilivyopo ni 8 tu.

Aidha amesema kuwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1087 hivyo hali ya upungufu wa vyumba vya madarasa inasababisha wanafunzi kusoma kwa kubanana katika madarasa yaliyopo hivyo wanaendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha wanakabiliana na upungufu

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top