Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WAZIRI MKUU MSTAAFU TANZANIA AKAMATWA NA JESHI LA POLISI GEITA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
  Jeshi   la   polisi    mkoani    Geita   limelazimika   kutumia   nguvu kwa   kupiga   mabomu   ya   machozi   ya   kutoa   m...



 

Jeshi  la  polisi   mkoani   Geita  limelazimika  kutumia  nguvu kwa  kupiga  mabomu  ya  machozi  ya  kutoa  machozi  kufyatua  risasi  za  moto  hewani  na  kupiga  virungu  wafuasi wa  chama  cha  demokrasia  na  maendeleo  chadema  waliokuwa   katika  stand  ya  mabasi  Geita  kwa  ajili  ya  kumpokea  Waziri  mkuu  mstaafu  na  mjumbe  wa kamati  kuu  ya  chama  hicho  EDWARD  LOWASSA  aliyewasili mkoani  humo kwa  ajili  ya  kampeini  za  uchaguzi  mdogo  katika  kata  ya  Nkome.

 


Tukio  hilo  limetokea   majira  ya  saa  kumi  jioni wakati  waziri   mkuu  huyo  wa  zamani  Edward   Lowassa akiwa kwenye gari  lenye namba  za  usajili T 771 DLA   akikatiza  katika  viwanja  vya   stand  ghafla  kikosi  cha  jeshi  la  polisi  kikiongozwa  na  mkuu wa  jeshi  hilo  wilayani  Geita  Ally Kitumbo  kufika  na  kuwatawanya  wananchi.
 

Katika  tukio  hilo  pia  waandishi  wa  habari  wawili   Vallency Robert  wa  Channel Ten na  Joel Maduka wa  kituo  cha  Redio  STORM FM  wamepigwa  na  kuharibiwa  vifaa  vyao vya  kazi.

Hata  hivyo licha  ya  Lowassa  kupelekwa  makao  makuu   ya  jeshi  la  polisi  mkoani  humo  kwa  ajili  ya kuhojiwa  haikuelezwa  mara  moja  sababu  ya jeshi  hilo  kutumia nguvu  kubwa.





 

Baadhi  ya  wananchi  waliozungumzia  tukio  hilo  wamelaani  matumizi  makubwa ya  nguvu ya   jeshi  la  polisi huku  wengine  wakilalamikia  waandishi  wa  habari  kuharibiwa  vifaa  vyao  na  kupigwa.


Pia  wananchi  hao  wamelaani  kitendo  hicho  kwa  kuwa  Lowassa  hakuwa  kwenye  mkutano  eneo  hilo  bali  alikuwa  akisalimiana  na  wananchi  wakati akielekea kwenye  kata  ya NKOME   kwa ajili  ya  kampeini za uchaguzi  mdogo.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top