Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WAZIRI LUKUVI ASEMA MIGOGORO YA ARDHI IMEPUNGUA KAGERA ASEMA SERIKALI IMEJIPANGA KUKOMESHA UJENZI HOLELA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Na: Sylvester Raphael Serikali katika Mkao wa Kagera yapunguza migogoro ya ardhi kwa kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya...
Na: Sylvester Raphael




Serikali katika Mkao wa Kagera yapunguza migogoro ya ardhi kwa kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu Tano changamoto kubwa  iliyobaki ni kupangilia miji na kuzuia ujenzi holela katika Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba.




Hayo yamesemwa leo Februari 19, 2018 na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Wiliamu Lukuvi mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera kwa ziara ya siku nne katika Wilaya za Bukoba (Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Manispaa ya Bukoa), Karagwe, Kyerwa na Ngara.

Mara baada  ya kupokea taarifa ya Mkoa ihusuyo Wizara yake kutoka kwa Mkuu wa Mkoa  wa Kagera Waziri Lukuvi aliwapongeza watendaji katika mkoa kuendelea kutatua migogoro ya ardhi na kutozalisha migogoro mipya bali migogoro iliyopo ni ile iliyozalishwa kipindi cha nyuma kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano haijaingia madarakani.



Waziri Lukuvi alisema kuwa Serikali iliamua kurasimisha maeneo ambayo tayari yalikuwa yamejengwa holela ili kupangilia miji lakini kuanzia sasa wananchi hawaruhusiwi kujenga holela na Watendaji wa Halmashauri hasa Maafisa wa Mipango Miji wanatakiwa kutoa Ramani za kila eneo kwa Watendaji wa Mitaa ili kuzuia ujengaji holela bila vibali vya ujezni vya Halmashauri husika.



“Kulikuwa na ucheleweshaji wa vibali vya ujenzi katika Halmashauri lakini kwa sasa Serikali imeamua kutoa kipengele cha vibali kupitishwa na Mabaraza ya Madiwani ili kuharakisha vibali vya ujenzi kutoka haraka kwa mwananchi anayetaka kujenga nyumba yake,” Alisistiza Waziri Lukuvi.


Katika kusisitiza suala hilo Waziri Lukuvi alisema kuwa Wataalamu wa Ujenzi, Mipango Miji na Mkurugenzi wanatakiwa kukaa na kupitia maombi ya vibali vya ujenzi na kutoa taarifa katika vikao vya Mabaraza ya Madiwani. Waziri Lukuvi alisema kuwa tayari Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI amesaini waraka wa kuondoa kifungu hicho ili vibali vipitishwe na Wataalam.


Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi alitoa rai kwa wananchi wa Kagera kuwa kuna wananchi mashamba yao yapo katika miji lakini hawataki yapimwe ambapo alitoa karipio kali kwa wananchi hao na kusema kuwa mpangaji wa ardhi ni Halmashauri, kama Serikali ikihitaji ardhi hiyo itamfidia mwananchi husika na kutumia ardhi hiyo kama ilivyopangwa

.

Pamoja na kutatua migogoro ya ardhi iliyoshindikana katikaHalmashauri za Wilaya zilizotajwa hapo juu Waziri Lukuvi pia atafuatilia suala la ulipaji wa kodi za ardhi katika maeneo atakayotembelea ili kona jinsi kodi hizo zinavyokusanywa na kuwahamasisha wananchi kulipa kodi hizo na Halmashauri kuchukua wajibu kikamilifu katika ukusanyaji.



Ikumbukwe kuwa katika Mkoa wa Kagera vimepimwa viwanja 2,897 kuanzia mwaka 2016 hadi kufikia sasa, aidha Halmashauri za Wilaya zote nane katika Mkoa wa Kagera zinaendelea na upimaji na kutao hati za viwanja.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top