Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WAZIRI NDALICHAKO AKIWA MKOANI KAGERA AAGIZA MAAFISA ELIMU NCHINI KUDAHILI WANAFUNZI KULINGANA NA UWEZO WA MIUNDOMBINU YA SHULE
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Na: Sylveste Raphael Waziara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako katika ziara yake ya sik...








Na: Sylveste Raphael



Waziara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako katika ziara yake ya siku mbili Mkoani Kagera kuanzia Februari 13 hadi 14, 2018 alitembelea, kukagua na kupokea  miradi mbalimbali ya Elimu  ikiwa ni pamoja na kutembelea baadhi ya shule za Sekondari na kuonge na wanafunzi wa shule hizo.



Wilayani Muleba
Katika siku yake ya kwanza Mkoani Kagera Prof. Ndalichako alitembelea na kukagua miundombinu ya Chuo cha Ualimu Katoke Wilayani Muleba ambapo katika chuo hicho ambacho miundombinu yake imechoka na alihaidi kuwa kitatengewa bajeti ya ukarabati kuanzia bajeti ya mwaka 2018/2019 ili kikarabatiwe.


Shule ya Sekondari Profesa Joyce Ndalichako, Prof. Ndalichako pia alifika katika shule hiyo iliyopewa jina lake ili kujionea ujenzi wa shule ambayo fedha zake zilitolewa na Serikali, Katika Shule hiyo Prof. Ndalichako aliridhika na viwango vya ujenzi wa shule hiyo na kuwapongeza wananchi kushirikiana na Serikali katika kujenga Shule hiyo.


Prof. Ndalichako aliwahasa wanafunzi kujitahidi katika masomo yao ili wasimwangushe kwani shule hiyo inaitwa jina lake. Pia alihaidi kutoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya kujenga Maabara na shilingi milioni 3 kwajili ya kununulia vitabu ili wanafunzi wa shule hiyo waweze kupata elimu stahiki.
Shule ya Sekondari Prof. Anna Tibaijuka Muleba mjini, katika ziara yake pia Prof. Ndalichako pia lipata wasaa wa kuitembelea Shule hiyo ambayo bado ina changamoto ya miundombinu kama madarasa pamoja samani za viti na meza kwa ajili ya wanafunzi .



Agizo;  Baada ya kuona msongamano wa wanafunzi katika shule hiyo Prof. Ndalichako alitoa Agizo kwa Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya Nchini kuacha tabia ya kudahili wanafaunzi  juu ya uwezo wa miundombinu katika shule husika. Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya popote nitakapokuta wamedahili watoto kuzidi uwezo wa miundombinu iliyopo watawajibika wao wenyewe, Alisistiza Prof. Ndalichako.



Prof. Ndalichako alisema kuwa ni ajabu kuona shule haina madarasa ya kutosha alafu Maafisa Elimu wanawapeleka wanafunzi wengi katika shule hiyo ambayo haiwezi kuwamudu wanafunzi hao kwa wakati mmoja. Katika hatua nyingine Prof. Ndalichako alihaidi kutoa  mabati 100 ili kumalizia chumba cha darasa ambalo ujenzi wake unaendelea.


Wilayani Missenyi
Siku hiyo hiyo akiwa Wilayani Missenyi Prof. Ndalichako alitembelea Chuo cha Maendelea ya Wananchi Gera na kujionea ukarabati wa Chuo hicho ambapo Serikali ilitoa Shilingi Milioni 75 ili kukarabati baadhi ya majengo. Prof. Ndalichako hakuridhishwa na kiwango cha ukarabati uliofanywa na VETA Kagera  katika chuo hicho kwani haundani na thamani ya fedha iliyotolewa.




Waziri Ndalichako aliwakemea VETA nchini kuwa  wamekuwa wakifanya kazi zao chini ya kiwango na alisema kuwa atatuma ukaguzi maalum katika Chuo hicho ili kukagua kazi iliyofanyika na kama ikigundulika kuwa kuna uchakachuzi VETA  Kagera watalazimika kukiarabati chuo hicho kwa gharama zao wenyewe, pia ukaguzi huo maalum utapitia na shughuli zao za kawaida kwani ilionekana kuwa wamekuwa wakifanya madudu.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top