Picha zinazomuonesha mwanamke aliyekutwa kwenye shimo la
mfanyabiashara mmoja jijini Dar es Salaam akiwa katika hali ya kutisha
zimetumiwa kufanya upotoshaji kwa kumzushia msichana mmoja wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Picha iliyounganishwa ikionesha taswira ya
msichana huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakidai kuwa hapo ni kabla
zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasio na nia njema na
kusababisha usumbufu kwa mrembo huyo.
Msichana huyo ambaye
anatumia jina la Ms.Adelaide kwenye Instagram amekanusha vikali taarifa
hizo huku akieleza kwa uchungu jinsi ambavyo ameathiriwa na uzushi huo.
“NAJUA
WENGI MTAKUA MMEKUTANA NA HIZI HABARI..SIJAJUA NANI ALIEANZISHA HII
MADA NA SIJUI IMEANZIA KWA NANI.
"MIMI NI MZIMA NA SIO MSUKULE JAMANI
NINA WAZAZI WOTE WAWILI WAPO HAI NA WAMEUMIZWA SANA NA HIKI KITENDO, MY
FAMILY MEMBERS WAMEUMIA MNOOO KUPITA KIASI
"LICHA YA HIYO MIMI BADO NI
MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU, WANAFUNZI WENZANGU WENYE MAPENZI NA MIMI
WANAUMIA SANA PIA WANAPOONA MAMBO KAMA HAYA.
"PLEASE ACHENI KUENDELEZA
HIZI HABARI ZA UONGO, TUSIPELEKANE MPAKA TCRA SASA MAANA TUTAKUA
TUNAPOTEZEANA MUDA,” aliandika Instagram.
Post a Comment