Mastaa wawili wenye majina makubwa Bongo ambao walikuwa wachumba walioshibana, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wanadaiwa kumwagana,
Habari
ya mjini kwa sasa ni juu ya wawili hao ambao walikuwa gumzo kwa watoto
wa mjini, kwa kila mmoja kuchukua hamsini zake na kufanya yake tofauti
na walivyokuwa awali huku chanzo cha kutengena kwao kikitajwa kuwa ni
wazazi wa sehemu zote mbili kutoridhiana.
Inadaiwa
kuwa, mbali na ishu ya wazazi, hivi karibuni Jokate na Kiba waliingia
kwenye gogoro kubwa la kimapenzi baada ya kufumaniana kwenye simu, jambo
ambalo limeendelea kutokea huku jamaa akiongoza kukutwa na meseji
kwenye simu yake za mwanamke mmoja anayedaiwa kuishi nje ya Tanzania.
“Ukisema
nikusimulie juu ya kumwagana kwa Jokate na Kiba basi tunaweza kukesha
ila mbali na mambo ya wazazi, kwa kifupi tu ni kwamba, hawa watu
wameingia kwenye mgogoro na kilichokuwa kikiwagombanisha mara nyingi ni
uhusiano wao wa zamani.”
“Mara
kadhaa Jojo (Jokate) amekuwa akimlalamikia jamaa (Kiba) kuwa ana demu
nje ya nchi ambaye amekuwa akimtundika katika mitandao ya jamii na
kujinadi kuwa ndiye mkewe tofauti na wengi wanavyojua kuwa Jokate ndiye
mtu wake.
“Mbali
na hilo, sasa kuna suala la familia zao kuonesha hali ya kutokubaliana
na wao kuoana hasa upande wa Jokate ambao ulionesha msimamo mkubwa
kutomtaka hata kidogo Kiba, mambo hayo yamekuwa ni chagizo kubwa katika
kuhatarisha mapenzi yao hivyo kufikia hatua hata ya wao kutoendelea
kupendana kwa dhati kama ilivyokuwa mwanzo wa penzi lao.”
“Tofauti
na watu walivyozoea kuwaona pamoja, kwa sasa wametibuana na hapa
tunapozungumza tayari kuna vikao kibao huko nyuma vilishakaa ili
kunusuru penzi lao lakini imeshindikana maana kila mmoja sasa hivi
anajifanyia mambo yake na hakuna dalili za kurudiana.
“Kiba anaonekana ameshajiingiza kwenye penzi la demu wake wa zamani huku Jokate naye akiwa ‘in love’ na mtu wake mwingine.”
“Kitambo
tu nimekuwa nikiwaambia kwa staili waliyokuwa nayo hakika wasingeoana
hata kama ukiweka pembeni suala la dini zao kutoendana, maana kuna siku
niliwasikia wakiambiana hata kama wazazi wakigoma wao wangefanya kila
juhudi hata wazae pamoja tu.
“Lakini
ukweli ni kwamba ilishindikana baada ya kuanza kugombana mara kwa mara,
pamoja na kwamba Jokate alikuwa akikubalika kwa asilimia zote kwa mama
Kiba na hata ndugu wengi wa Kiba walionekana kumpenda waziwazi,” kilisema chanzo .
Alipotafutwa
Ali Kiba ili atoe la moyoni juu ya madai hayo ya kumwagana na Jokate
alisema kuwa haoni sababu ya kuzungumzia ishu hiyo kwani ni mambo
binafsi.
Post a Comment