Home
»
»Unlabelled
» UPDATES ZA HABABARI YA AJALI HII MSAFARA WA RAIS DKT JOHN MAGUFULI UMEPATA AJALI ASKARI WATATU WAFARIKI NA
Habari za hivi punde zilizoufikia mtandao huu wa Karagwe Forum zinaeleza kuwa msafara wa Rais John Magufuli umepata ajali eneo la Manyoni Mkoani Singida ukiwa njia ukitokea mjini Singida ambapo maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM kitaifa zilifanyika .
Tutakujuza kadri tutakapovyopata taarifa.
UPDATES ZA HABABARI YA AJALI HII
Rais Magufuli alikuwa mjini Singida alikokuwa amekwenda kushiriki maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
Hiyo
ni mara ya pili kwa askari kufariki wakiwa kwenye msafara wa Dk
Magufuli baada ya aliyekuwa akiongoza msafara wake wakati wa kampeni
kugongana na dereva bodaboda katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.
Askari
huyo alikuwa kwenye pikipiki maalumu iliyokuwa ikiongoza msafara wakati
Dk Magufuli akitoka katika Hospitali ya Lugalo kuaga mwili wa aliyekuwa
mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka alisema ajali hiyo
ilitokea saa 9.40 alasiri, katika Kijiji cha Isuna, Wilaya ya Ikungi
mkoani humo baada ya moja ya matairi ya gari hilo kupasuka na dereva
kushindwa kulimudu.
Aliwataja waliofariki kuwa ni Mkaguzi Mwajelo, Sajenti Elias Mrope na Sajenti Gerard.
Waliojeruhiwa ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Singida (RCO), Peter Majira (50
na PC Charles Simon (34) ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.
Gari
hilo lililopata ajali ni lile lililokuwa limetangulia ili kufagia
barabara kabla ya msafara wa Rais, likiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha
Usalama Barabarani cha mkoa huo.
Sedoyeka alisema miili ya askari hao imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya mkoa huo.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Kitundu Jacks alisema hali
za majeruhi waliofikishwa kwenye hospitali hiyo zinaendelea vizuri.
“Mrope
ndiye aliyeletwa akiwa kwenye hali mbaya, alikuwa amevunjika mbavu na
mkono na akafa mara tu baada ya kufikishwa hospitalini hapa. Majeruhi
wengine wamepata michubuko na wanaendelea vizuri,” alisema.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Recent Posts
- ADC Summit 2025!09 Jan 20250
The African Disability Collaboration (ADC) is thrilled to host the ADC Summit 2025 under the ...Read more »
- KAGERA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KUENDELEA KUJIIMARISHA KUWALINDA RAIA NA MALI ZAO25 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Vyombo ya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera vyafanya mazoezi ya ...Read more »
- MBIO ZA MWENGE WA UHURU KATIKA WILAYA ZA KARAGWE NA NGARA PIA HITIMISHO WILAYANI BIHARAMULO MKOANI KAGERA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mwenge wa Uhuru waendelea kuchanja mbuga Mkoani Kagera kwa ku...Read more »
- MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI KAGERA NA KUANZA UZINDUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YABILIONI 1216 Apr 20180
Na: Sylvester Rapahel Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo April 8, 2018 Mkoani Kagera na...Read more »
- TIMU YA WATAALAM WA UJENZI KUTOKA NCHINI CHINA YAKAGUA ENEO LA UJENZI WA CHUO CHA VETA KAGERA ILI KUANZA UJENZI MARA MOJA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Serikali ya Watu wa China yatuma timu ya Wataalam wa Usanif...Read more »
- MKOA WA KAGERA WAVUKA LENGO KATIKA UNDIKISHAJI WA WANAFUNZI AWALI NA DARASA LA KWANZA MWAKA 201816 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mkoa wa Kagera wavuka lengo la uandikishaji wa Wananfunzi katika madarasa...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.