Jamii imetakiwa kutambua
umuhimu wa uhai wa mwanadamu tangu inapotungwa mimba hadi kuzaliwa kwa kuepuka baadhi ya vitu vinavyosababisha
kuondoa uhai wa mwanadamu ikiwemo madawa ya kupanga uzazi utoaji mimba,na
magonjwa ya zinaa.
Hayo yamesema na Mwezeshaji Emili Agamu katika semina juu ya utetezi wa uhai iliyofanyika
katika makao makuu ya Jimbo Katholiki la Kayanga ikihusisha wajumbe kutoka
Dekania ya Bugene ambayo inaundwa na parokia za Ndorage,Bugene, na Parokia ya
Mtakatifu George.
Agamu amesema kuwa mwanzo wa
uhai wa mwanadamu uko mikononi mwa Mungu na anayeamua kuondoa uhai huo ni Mungu
pekee lakini katika dunia ya sasa binadamu wamechangia katika kuondoa uhai wa
binadamu wenzao kwa kutumia madawa ya
kuzuia mimba yaani Vidhibiti mimba,magonjwa ya zinaa na sababu nyinginezo
ambapo amesema kuwa hayo yote ni chukizo kwa Mungu na sio maelekezo ya Kanisa
katholiki.
Amesema kuwa sababu nyingine
ya kutoa uhai wa mwanadamu ambayo kwa sasa imeshamili ni utoaji wa mimba ambapo
wanaofanya hivyo hudai kuwa wanapanga uzazi,hali ngumu ya maisha na sababu
nyingine kama za kubakwa .
Agamu ametaja madhara mbalimbali ya kutoa mimba yakiwemo ya
kimwili, kiakili na kiroho ambapo amezitaka familia kuachana na vitendo
hivyo viovu kwani kwa kufanya hivyo unakuwa umeondoa uhai wa binadamu na
ukizingatia kuwa mwenye uwezo wa kuondoa uhai ni Mungu pekee.
Kwa upande wake Askofu
Almachius Vicent Rweyongeza amesema kuwa wakristo wengi sasa wanaharibu miili
yao kwa namna mbalimbali ambapo amewataka kumrudia Mungu na kuachana na anasa
za hapa duniani.
Semina hii ya utetezi wa
uhai itaendeshwa kwa Dekania nne ambazo ziko ndani ya Jimbo hili la Kayanga.
Post a Comment